Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya DCB Bw. Godfrey Ndalahwa wakati akizungumza na hiyo waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu mafanikio ya benki hiyo ikiwa katika maadhmisha ya kutimiza miaka 20 tokea kuanzishwa kwake kulia ni Mkuu wa Masoko na Mawasiliano Rahma Ngasa.
Jumla ya mikopo yenye thamani isiyopungua trilioni 1 imenufaisha watanzania wasiopungua 400,000 ambapo pia Benki imeweza kupunguza mikopo chechefu kutoka asilimia 11.6 mwaka 2020 hadi kufikia asilimia 7.3 mwaka 2021.
Hayo yamebainishwa Jijini Dar es Salaam leo na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya DCB Bw. Godfrey Ndalahwa wakati akizungumza na hiyo waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu mafanikio ya benki hiyo ikitimiza miaka 20 tokea kuanzishwa kwake.
Amesema jambo lingine ni Kuongeza kiwango cha faida kinachopatikana kila mwaka hadi kufikia kiasi cha shilingi bilioni 11 mwaka 2025 na kuongeza idadi ya wateja hadi kufikia wateja 400,000 ifikapo mwaka 2025.
Ameongeza kuwa Benki hiyo inakwenda kuonesha taswira mpya ya mafanikio yake kuelekea mwaka 2025 ikiwemo kuongeza kiwango cha faida kinachopatikana kila mwaka hadi kufikia kiasi cha shilingi bilioni 11 mwaka 2025.
“Uetekelezaji huo una vipaumbele vitano vitakavyofanikisha taswira mpya ya mafanikio: hayo ambavyo kukuza kiwango cha mikopo kwa wateja kutoka kiasi cha shilingi bilioni 104 mwaka 2020 hadi kufikia shilingi bilioni 290 mwaka 2025 na kupunguza mikopo chechefu hadi kufikia chini ya asilimia 5,” amesema Ndalahwa.
Ameongeza kuwa mwaka 2021 benki hiyo imefanikiwa kukuza mikopo yake hadi kufikia shilingi bilioni 121 ambayo ni sawa sawa na ongezeko la asilimia 16 kwa mwaka.
Mengine yaliyoainishwa ni kutoa huduma bora zaidi kwa wateja na hivyo kuongeza idadi ya wateja hadi kufikia wateja 400,000 ifikapo mwaka 2025 na kuongeza ufanisi na udhibiti wa mali za benki
Aidha, Mkurugenzi huyo alisema kuwa Benki yake inalenga kuongeza mchango wa amana za gharama nafuu katika amana zote za benki kutoka asilimia 34 mwaka 2020 hadi kufikia asilimia 60 ifikapo mwaka 2025.
Aliongeza kuwa nia ya lengo hilo ni kupunguza gharama zitokanazo na amana za muda maalumu (Fixed Deposits), ambapo itaongeza faida na kuleta ongezeko la thamani kwa wanahisa.
“DCB itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita ya Raisi Samia Suluhu Hassan katika azma yake ya kuwainua watanzania kiuchumi na kuchangamkia pia fursa za kifedha zitokanazo katika miradi mbalimbali ya kimaendeleo inayoendelea hapa nchini,”amesema.