Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Dkt. Noel Lwoga akionyeshwa jambo na Mama wa kimila Bi. Elda P. Maka wakati alipotembelea katika Maonyesho ya Kimataifa ya 46 ya Biashara maarufu kama Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwl. Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es SalaamMkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Dkt. Noel Lwoga akiwa amekaa na kuzungumza na Mzee wa kimila Willy B. Nyamtiga wakati alipotembelea katika Maonyesho ya Kimataifa ya 46 ya Biashara maarufu kama Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwl. Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es SalaamMkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Dkt. Noel Lwoga akishiriki kucheza mchezo wa bao na Rais wa Bao Monday M. Likwepa wakati alipotembelea katika Maonyesho ya Kimataifa ya 46 ya Biashara maarufu kama Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwl. Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam
Picha ya pamoja
………………….
Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Dkt. Noel Lwoga amewakaribisha wawekezaji mbalimbali kuwekeza katika maenwo ya makumbusho na malikale.
Dkt. Lwoga ametoa wito huo katika Maonyesho ya Kimataifa ya 46 ya Biashara maarufu kama Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwl. Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam. yenye kaulimbiu “Tanzania ni Mahali Sahihi kwa Biashara na Uwekezaji
Amesema Makumbusho ya Taifa inayosimamia makumbusho na malikale nchini ina maeneo mbalimbali ambayo wadau wanaweza kuwekeza ikiwa ni pamoja na maeneo ya migahawa, hoteli, jukwaa la sanaa (theater), studio, maduka ya zawadi, viwanja, mashine ya kutolea fedha (ATM) na makambi ya muda (cape site).
“Tunatoa wito kwa wadau wa uwekezaji kuja kuwekeza katika maeneo ya makumbusho na malikale ambapo kuna fursa nyingi na vituo vyetu vingi viko mjini. amesema Dkt. Lwoga