Wachezaji wa timu teule ya Mpira wa Kikapu ya jeshi la Ulinzi wa wananchi wa Tanzania wameagwa rasmi katika viwanja vya Don Bosco (Oyster bay) Jijini Dar es salaam kuelekea Nchini Ujerumani katika Mashindano ya Majeshi duniani.
………………………
Timu Teule ya Mpira wa Kikapu Ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania imeagwa rasmi Jana Katika Viwanjani Vya Don Bosco( Oysterbey) Jijini Dar es salaam kuelekea Nchini Ujerumani katika Mashindano Ya Majeshi Duniani ya Wachezaji watatu watatu.
Akizungumza katika Hafla hiyo katibu wa Chama Cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (DABA )Mpoki Mwakipake amesema Familia ya Kikapu inawataakia heri katika Mashindano hayo kwa kuwa inawakilisha Mkoa Jeshi na Taifa kwa Ujumla.
” Hawa Ni Wachezaji wanatoka kwenye Ligi ya Mkoa wa Dar es Salaam Ni fahari Jeshi Kuona wanayo sifa ya kushiriki Mashindano hayo”
Kwa Upande wake Meneja wa timu hiyo Kapteni Mohamed Kasui alisema maandalizi yamekamilika kwa asili mia moja huku wakiahidi kurudi na Ushindi.
Alisema Mashindano hayo ya Wachezaji watatu watatu Three On Three World Championship yatakishirikisha Nchi Takribani 26 zikiwemo za
Bara la Ulaya, Asia na Afrika.
Timu hiyo inajumuisha Wachezaji kumi wakiwemo Wanawake na Wanaume Viongozi.
alitaja Wachezaji hao kuwa ni Kocha Sajini Taji Haleluya Kavalambi
Sajini Faraja Malack
Koplo Mpala Sadick
Koplo Baraka Athumani
Koplo Penina Lushinge
Private Mosez Jackson
Private Selina Msingwa
Private Enerico Maengela na Private Alinani Msongole.
Kwa Upande wa Manahodha wa Timu zote Mbili Faraja Malaki nahodha Wanawake na Baraka Sadick Nahodha Wanaume kwa Nyakati tofauti wameahidi kujituma na kutafuta Ushindi.