Katibu Mkuu Maliasili na Utalii , Profesa Emanuel Sedoyeka akikata utepe pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP Tanzania, Ndg. Christine Musisi wakati mwakilishi huyo alipokabidhi magari 10 aina ya Land Cruiser leo Julai 2, 2022 Jijini Dar es Salaam Kwa ajili ya mradi wa kupambana na ujangili katika mbuga za wanyama.
Katibu Mkuu Maliasili na Utalii , Profesa Emanuel Sedoyeka akijaribu kuliendesha moja ya magari 10 yaliyokabidhiwa kwa wizara hiyo leo na UNDP.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP Tanzania, Ndg. Christine Musisi akijaribu kuliendesha moja ya magari 10 aliyoyakabidhi kwa wizara ya Maliasili na Utalii.
Katibu Mkuu Maliasili na Utalii , Profesa Emanuel Sedoyeka akikata utepe pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP Tanzania, Ndg. Christine Musisi wakizungumza na waandishi wa habari.
Katibu Mkuu Maliasili na Utalii , Profesa Emanuel Sedoyeka akikagua kikosi cha Jeshi Usu na kupokea heshima mara baada ya kuwasili katika ofisi ndogo ya Wizara ya Maliasili jijini Dar Es Salaam.
Mgari 10 yaliyokabidhiwa leo.
………………………….
Wizara ya Maliasili na Utalii imepokea magari kumi yaliyotolewa na UNDP kwaajili ya kuongeza nguvu ya serikali katika jitihada za kupambana na ujangili wa wanyamapori
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa magari hayo, Katibu Mkuu Maliasili na Utalii , Profesa Emanuel Sedoyeka amesema Magari hayo yanakwenda kwenye kaya 10 tofauti tofauti Tanzania lengo ni kuhakikisha kwamba rasilimali zinalindwa;
“Nchi yetu ipo katika mapambano makali dhidi ya ujangili na kulinda rasilimali za nchi hii na sisi kama wizara ya maliasili tumekabidhiwa majukumu ya kuhakikisha kwamba majukumu hayo yanaendelea vizuri na rasilimali zetu zinaendelea kutumika vizuri katika Taifa na kubaki kwaajili ya vizazi vijavyo” Alisema Sedoyeka na kuongeza kuwa;
“Ili kujengea uwezo timu yetu mahususi ya kupambana na ujangili ilionekana kwamba walitakiwa waongezewe vitendea kazi ambapo leo tumezindua magari haya kumi”
Pia Sedoyeka amesema Idadi ya wanyama wetu wakubwa kama Tembo, Nyati, Kifaru n walikuwa wakipungua lakini baada ya jitihada hizo kwa sasa wamekuwa wakiongezeka.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Tanzania,Bi. Christine Musisi amesema UNDP imeamua kuchangia juhudi za serikali za kupambana na ujangili wa wanyama pori kutokana na sekta ya utalii kuwa mstari wa mbele katika kukuza uchumi wa nchi.