……………………
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
MKUU wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge, amepokea na kukabidhi mitambo ya kusafisha Maji chumvi(Solar Desalination System) ,zenye thamani ya Shilingi Milioni 700 zitakazo tumika katika Hospital ya Wilaya ya Mafia na Kibiti.
Akipokea Mitambo hiyo katika Kituo cha MEDEWEL Kibaha Kunenge amesema
“Namshukuru Rais Samia Suluhu Hassan Kwa kuweka Mazingira bora kabisa ambapo sekta binafsi na wadau mbalimbali wanashirikiana na Serikali katika kutoa huduma kwa Wananchi”
Ameeleza kupitia Juhudi hizo katika Mkoa wa Pwani wamepokea mitambo ya kusafisha Maji chumvi kutoka kwa WaterKiosk na Boreal light yenye makazi yake Nchini Ujerumani kwa ufadhili wa benk ya Ujerumani.
“Mitambo hii itasaidia kusafisha maji chumvi kutoka katika visima vyetu kuhakikisha yanakuwa katika hali ya kutumika”
Ameeleza kuwa ni “Mitambo hii ni mizuri na kwamba ni Teknolojia rahisi na inatumia nguvu ya jua ambayo haina athari katika mazingira .
Ameeleza kuwa Serikali inafanya Jitihada kubwa kuhakisha maeneo yote yanapata Maji na kwa Mkoa wa Pwani “Upatikanaji wa Maji ni wastani asilimia 86 na tunalengo ifikapo 2025 mijini Upatikanaji wa Maji uwe Asilimia 95 na Vijijini Asilimia 85.