Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko Chuo Kikuu cha Mzumbe Rose Joseph (kulia) akifafanua jambo kwa mgeni aliyefika kwenye Banda la Chuo hicho kupata maelezo mbalimbali kuhusu Chuo hicho. (katikati) ni Happiness Chilewa Afisa Uhusiano Mkuu Ndaki ya Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko Chuo Kikuu cha Mzumbe Rose Joseph (kushoto) akijadiliana jambo na Maofisa wa Chuo hicho katika Banda lao. (kulia) ni Mratibu wa Udahili Dr. Michael Mangula na (katikati) ni AfisaUdahili Isaac Msengi
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko Chuo Kikuu cha Mzumbe Rose Joseph (kushoto) akimpa maelezo kuhusu kozi mbalimbali zinazotolewa na Chuo hicho kwa Mwandishi wa Habari Mwandamizi na Mkurugenzi wa Blog ya Fullshangwe John Bukuku (kulia) aliyefika katika Banda la Chuo hicho kupata Habari.
Afisa Udahili wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Brandina Elisa (kushoto) akifanya udahili kwa mhitimu waKidato cha sita Mwajuma Zwili (kulia) aliyetembelea Bandani hapo kwaajili ya kupata ushauri na kufanya udahili, katika maonesho ya sabasaba Jijini Dar es Salaam.
Mhadhili Msaidizi wa Sheria Chuo Kikuu Mzumbe Deogratiuas Mapendo (kulia) akiwa na Mratibu wa Kituo cha Msaada wa sheria Bernadetha Iteba (katikati) na james Marandu (kulia) wakiwa tayari kutoa huduma Bandani hapo hapo. PICHA NA: HUGHES DUGILLO
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Elimu kwa Umma Chuo Kikuu Cha Mzumbe Bi. Rose Joseph amesema kuwa katika mwaka mpya wa masomo unaotarajiwa kuanza hivi karibuni Chuo hicho kimeanzisha Programu mya tano zitakazotolewa kuanzia hatua ya Cheti hadi Shahada ya juu ya Uzamivu.
Bi. Rose ameyasema hayo Julai 1,2022 katika mahojiano maalum na waandishi wa habari katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam ambapo Chuo hicho kimeweka kambi kikishiriki maonesho hayo kwaajili ya kutoa huduma mbalimbali na kufanya udahili wa papo kwa hapo.
Aidha ameeleza kuwa pamoja na Programu hizo pia chuo hicho kimeanzisha Miradi mbalimbali ya kusaidia jamii pamoja na kutoa msaada wa Kisheria ambapo wananchi wanapatiwa msaada wa kisheria katika banda lao.
“Chuo Kikuu Mzumbe tumekuja na vitu vingi kwenye maonesho ya mwaka huu kuna miradi mbalimbali hapa ikiwemo ya ufugaji kwa kutumia mbinu za kisasa na mradi wa utunzaji wa mazingira” amesema Rose.