Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akizindua mitambo ya kuzalisha hewa tiba ya Oksjeni iliyogharimu bilioni 1.5 ambapo zimetumika kununua mitambo, gari ya kusambazia mitungi ya oksijeni, mitungi 560 pamoja na ujenzi wa jengo ambalo mitambo hiyo imefungwa.waziri ummy mwalimu akiangalia mitambo hiyoWaziri ummy mwalimu akiwasha mitambo hiyo ya kuzalisha hewa tiba ya oksijeni ambao unazalisha mitungi 400 kwa siku na ina sehemu mbili ambazo hazitegemeani, hivyo kuweza kuwasha sehemu moja kipindi mahitaji yanaposhuka na pia kuhakikisha uzalishaji unaenendelea wakati wote hata wakati wa matengenezo kinga inapolazimu kuzima upande mmoja. jengo la mitambo ya kuzalisha hewa tiba ya oksijenmi iliyojengwa kwenye hospitali ya kanda ya Benjamin MkapaWaziri wa Afya Ummy Mwalimu akizindua kitabu cha mwongozo wa utoaji dawa (Benjamin Mkapa Hospital Formulary ) utakaotumiwa na waandika dawa (Prescribes), wafamasia, wachunguzi na wauguzi.Baadhi ya mitungi ya gesi iliyoko kwenye jengo hilo(Picha zote na Engliberth Kayombo)Picha ya pamoja ya Waziri wa Afya Ummy mwalimu, mwenyekiti wa bodi ya udhamini wa hospitali hiyo dkt. deo Mtasiwa(kushoto),mkurugenzi mtendaji wa Hospitali hiyo Dkt. Alphonce Chandika(Kulia) pamoja na viongozi wa Wizara ,hospitali na wajumbe wa bodi ya hospitali mara baada ya uzinduzi wa mitambo hiyo.
……………………………..
Na.Catherine Sungura,WAF-Dodoma
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amezindua mitambo wa hewa tiba ya Oksijeni wenye thamani ya bilioni 1.5 kwenye hospitali ya Benjamnin Mkapa iliyoko jijini Dodoma.
Waziri Ummy amesema usimikaji wa mitambo hiyo ni sehemu ya mikakati ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kuhakikisha kuwa huduma zinaboreshwa na kuongeza kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja mitambo 14 imeshasimikwa kwenye hospitali za rufaa za mikoa nchini.
“Sisi kama Sekta tumejiwekea vipaumbele vyetu ambavyo Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ingependa kuviona tunavitekeleza, kipaumbele kikubwa ni ubora wa huduma za afya, hivyo mitambo hii ina lengo la kuokoa maisha kwa wananchi wake”.
Waziri Ummy amesema wanatarajia kusimika mitambo mingine 57 ya hewa tiba ya Oksijeni kwenye hospitali za rufaa za mikoa,Kanda pamoja na Wilaya nchini.
Aidha, Waziri Ummy ameipongeza hospitali hiyo pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Dkt.Alphonce Chandika kwa kuhakikisha kuwa kazi ya usimikaji wa mitambo huo unakamilika kwa wakati na unazingatia viwango vinavyotakiwa
Ameongeza kuwa mitambo hiyo haitosaidia hospitali hiyo tu bali hata hospitali na vituo vya mikoa wa Dodoma na mikoa ya jirani ikiwemo Manyara, Singid na Iringa.
Pia amesema licha ya mitambo huo ambao ni mradi mmoja kati ya miradi 17 ambayo inatekelezwa na Rais Samia Suluhu Hassan ambapo jumla ya takribani Bilioni 10.02 zimeelekezwa katika kukamilisha miradi hiyo hospitalini hapo.
Naye,Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo Dkt. Alphonce Chandika amesema mitambo hiyo inazalisha mitungi 400 kwa siku na una sehemu mbili ambazo hazitegemeana hivyo unaweza kuwasha sehemu moja kipindi unatumia ili kuhakikisha uzalishaji unaendelea wakati wote hata wakati wa matengenezo kinga inapolazimu kuzima upande mmoja.
Dkt.Chandika aliongeza kabla ya hapo hospitali ilikua ikitumia mitungi 200 kwa mwezi lakini kipindi cha UVIKO-19 matumizi yakiongezeka hadi kutumia mitungi 200 kwa siku na hivyo kuongeza gharama za uendeshaji wa hospitali na kutumia milioni 10 kwa siku badala ya milioni 10 kwa mwezi kwa kipindi hicho cha UVIKO-19.
Bilioni 1.5 zimetumika kununua mitambo miwilli aina ya Ozcan Kardesler Tip Cihazlari San,mitungi ipatayo 560 ya hewa tiba,gari la kusambazia mitungi ya Oksijeni pamoja na ujenzi wa jengo ambalo mitambo imefungwa.