Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju akizungumza na Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii Dkt.Joyce Nyoni wakati alipowasili kwenye banda la taasisi hiyo kwenye maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Julai 1,2022.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju akizungumza na Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii Dkt.Joyce Nyoni wakati alipowasili kwenye banda la taasisi hiyo kwenye maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba leo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju akipata maelezo kutoka kwa watumishi wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii wakati alipotembelea kwenye banda la taasisi hiyo katika maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba leo.
Baadhi ya wananchi wakipata maelezo kutoka kwa wafanyakazi wa taasisi hiyo wakati walipotembelea katika banda hilo.
……………………………………..
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju amesema tunapoongelea ustawi wa jamii ni ustawi wa kila kitu wakiwemo wanawake, watoto, vijana ,wazee pamoja na makundi maalum
Tuko katika maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba ili kuwaelimisha wananchi maendeleo yanaanza na mtu mmoja, Watu kisha nchi kwa ujumla na kwamba ustawi wa jamii siyo lazima uajiliwei namna utakavyojitambua na kuchukua hatua ili kujiletea maendeleo.
Amesema Elimu inayotolewa kwa wananchi katika maonesho ya sabasaba ni ustawi wa jamii kuhusu malezi ustawi wa familia , ustawi wa ndoa Ustawi wa watoto Maofisini na maeneo mengine ambayo ni muhimu kwa ustawi wa jamii kwa ujumla.
“Tunaamini kwamba pasipokuwa na migogoro taifa litakuwa na amani ya kutosha na litapiga hatua katika maendeleo hivyo tunawakaribisha watu wote katika banda letu ambapo watapata ushauri nasaha na namna ya kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa watoto na wanawake lakini namna ya kupambana na ukatili huo,” Amesema Amon Mpanju.
Naye Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii Dkt.Joyce Nyoni amesema Kikosi maalum kilichopo katika Taasisi ya Ustawi wa Jamii Kijitonyama kipo Sabasaba kwa ajili ya kutoa msaada wa elimu na maarifa namna ya kupambana na changamoto za mahusiano katika jamii pamoja na msaada wa kisaikolojia ambao utatolewa kwenye viwanja vya sabasaba.
Ameongeza kwamba atakayefika katika banda la taasisi hiyo na kupata huduma zinazotolewa hapo na wataalamu wao hatajuta kufika hapo bali atafurahia na kutamani kurudi tena bandani hapo ili aweze kupata mambo mazuri zaidi kuhusu masuala ya mahusiano na saikolojia pamoja na kupata mbinu za utatuzi wa changamoto hizo.