Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation, Dkt. Ellen Mkondya – Senkoro akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Jukwaa la kumbukizi ya pili ya aliyoyafanya na kuacha alama muasisi wa Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation, Rais wa Awamu ya Tatu, Hayati Benjamin William Mkapa ambalo linatarajia kufanyika Zanzibar Julai 13 na 14 2022 Zanzibar.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation, Dkt. Ellen Mkondya – Senkoro akifafanua jambo hukuhusu Jukwaa la kumbukizi ya pili ya aliyoyafanya na kuacha alama muasisi wa Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation, Rais wa Awamu ya Tatu, Hayati Benjamin William Mkapa ambalo linatarajia kufanyika Zanzibar Julai 13 na 14 2022 Zanzibar.
JUKWAA la kumbukizi ya pili ya aliyoyafanya na kuacha alama muasisi wa Taasisi ya wa Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation, Rais wa Awamu ya Tatu, Hayati Benjamin William Mkapa linatarajia kufanyika Zanzibar Julai 13 na 14 2022.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo Juni 29, 2022, wakati wa kutambulisha kumbukizi ya pili, Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation, Dkt. Ellen Mkondya – Senkoro amesema kuwa Jukwaa hilo limepangwa kufanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Airport, Zanzibar.
Kauli mbiu ya Jukwaa hilo ni “Uongozi Madhubuti Hamasa ya Mabadiliko kwa Wote.” (Resilient Leadership- Inspiring Change for All).
Jukwaa au Mdahalo huo wa siku mbili utaanza saa Mbili asubuhi na unatarajia kumalizika saa nane mchana huku wageni waalikwa takriban 500 watahudhiria Siku ya kwanza mdahalo utafunguliwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Othman Masoud.
Na siku ya pili ya Julai 14,2022 itakuwa siku ya kilele cha mdahalo huo kwa mwaka 2022, na Mgeni rasmi katika siku hii muhimu atakuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.
Dkt. Ellen amesema kuwa Katika siku hizo mbili kutakuwa na mdahalo kuhusu mada kuu mbili ambazo ni
1.Kuongoeza kasi katika mikakati ya mabadiliko katika mifumo ya afya Tanzania kupitia biashara ushirika, (Accelerating Strategic Health Transformation in Tanzania through Business Coalition)
2.Ubunifu katika miradi na mikakati yaa ushirikiano kati ya Serikali, Taasisi za umma na za binafsi katika kuleta huduma ya afya kwa wote. (Innovative Public-Private Partnerships (PPP) approaches towards attaining Universal Health Coverage)
“Kupitia mada hizi washiriki watapata fursa ya kusikia mijadala ya juhudi za mashirikianao ya Serikali za Tanzania Bara na Visiwani, Sekta binafsi na Wadau wa maendeleo na pia iliyoendelea kuchagizwa na Taasisi ya Benjamin Mkapa, katika kuimarisha mifumo ya afya kwa lengo la kuhakikisha kila mtu popote alipo anapata fursa ya kupata huduma bora za afya. Mjadala huu pamoja na mambo mengine utashirikisha jopo la wadau watakao chambua kwa undani umuhimu wa biashara ama uwekezaji wa pamoja katika kuinua afya na ustawi wa kila mmoja wetu.” Amesema Dkt. Ellen
Viongozi wengine wa kitaifa watakaohudhuria mdahalo huu ni pamoja na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi, Daktari Hussein Ali Mwinyi, ambae pia ni “msarifu” wa Taasisi ya Mkapa Foundation, aliyerithi nafasi ya Hayati Benjamin Mkapa katika Taasisi yetu kuanzia Desemba 2021.
Wageni wengine watakaoshiriki hafla hii ni pamoja na Viongozi wakuu wa Serikali, Marais na Viongozi wastaafu kutoka Tanzania Bara na Visiwani, Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini, Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa hapa Nchini, Wakuu wa Taasisi mbalimbali za Sekta binafsi na za Umma,Wanafamilia na Marafiki wa Hayati Benjamin Mkapa kutoka ndani na Nje ya Nchi, pamoja na Asasi za kiraia na Viongozi wa dini.
Tunapenda kutoa shukrani kwa wadau wote ambao wapo Pamoja na sisi katika maandalizi ya kufanikisha mdahalo huu wa kumbukumbu na kuenzi Maisha ya Hayati Mheshimiwa Benjamin William Mkapa,Rais wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri wa Muungano ya Tanzania na Msarifu wa Taasisi Benjamin William Mkapa