Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro(Mb) amewahakikishia Baraza la Uongozi la Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) ushirikiano kutoka Serikalini kupitia Wizara ya Katiba na Sheria.
Dkt. Ndumbaro ameyasema hayo leo tarehe 24 Juni, 2022 Jijini Dodoma, wakati wa mazungumzo na Baraza la Uongozi la Chama cha Wanasheria wa Tanganyika wakiongozwa na Rais wa chama hicho, Prof. Edward Hosea.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Geofrey pinda amewapongeza viongozi wa TLS kwa kuaminiwa na kuwataka wawatumikie wanachama kwa juhudi na ubunifu ili kuleta mabadiliko chanya.
Naye Katibu Mkuu, Bi. Mary Mkondo amesema milango ya Wizara ipo wazi muda wote kwa jambo lolote litakalo hitaji ushirikiano ili kuleta maendeleo kwa wananchi na kuzingatia Haki.
Rais wa TLS, Prof. Edward Hosea ameishukuru Serikali kwa utayari wake wa kushirikiana TLS katika mambo mbalimbali yaliyo ainishwa kweye kikao hicho, ikiwa ni pamoja na kutoa huduma ya msaada wa kisheria na maendelea ya kituo cha pamoja cha usuluhishi.