Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godwin Gondwe akizungumza kwenye tamasha maalum la kuwapa fursa watoto wa Tanzania wenye mahitaji maalum ambalo limefanyika katika Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es salaam.
Muhifadhi Mila Mwandamizi wa kijiji cha Makumbusho na Kaimu Mkurugenzi Kijiji hicho Wilberd Lema akieleza dhamira ya Makumbusho kufanya tamasha hilo mara kwa mara hasa kwa kuwa karibu na watoto wenye uhitaji maalum.
Afisa Elimu wa Makumbusho ya Taifa na Mratibu wa Tamasha la Watoto wenye mahitaji maalum kwa Mwaka huu Wilhelmina Joseph akifanya mahojiano na waandishi wa habari.
Mwanafunzi Theresia Fredrick kutoka Shule ya Jeshi la Uokovu ya jijini Dar es salaam akieleza furaha yao katika tamasha hilo.
Mkuu wa Idara ya Program Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Chance Ezekiel akisherehesha tamasha hilo maalum la kuwapa fursa watoto wa Tanzania wenye mahitaji maalum ambalo limefanyika katika Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es salaam.
Picha ya Pamoja (picha zote na Mussa Khalid)
……………………..
NA MUSSA KHALID
Maafisa elimu na Maafisa ustawi wa Jamii katika Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam wametakiwa kupita mara kwa mara katika shule ambazo watoto wanabainika kuwa na matatizo ya mahitaji maalum ili waweze kupatiwa matibabu kwa haraka.
Kauli hiyo imetolwa leo jijini Dar es salaam na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godwin Gondwe wakati akizungumza kwenye tamasha maalum la kuwapa fursa watoto wa Tanzania wenye mahitaji maalum ambalo limefanyika katika Kijiji cha Makumbusho.
Mkuu wa Wilaya Gondwe amesema Wilaya hiyo itaanza kufanya kampeni ya nyumba kwa nyuma ili kuangalia watoto wanaofichwa majumbani waweze kupatia elimu itakayo wasaidia kwenye maisha yao.
‘Mimi nakemea ukatili kwa watoto wenye mahitaji hapana hivyo wito kwa wazazi wakae karibu na watoto wao na sio wawaachie wafanyakazi wa Nyumbani kwani wengi wao wamekuwa wakibainika kuwawafanyia ukatili watoto na kutokomea’amesema DC Gondwe
Awali akizungumza Muhifadhi Mila Mwandamizi wa kijiji cha Makumbusho na Kaimu Mkurugenzi Kijiji hicho Wilberd Lema amesema lengo la kuandaa tamasha hilo ni kuonyesha fursa kwa watoto wenye uhitaji maalum kuelimika na shughuli za makumbusho.
Kwa upande wake Afisa Elimu wa Makumbusho ya Taifa na Mratibu wa Tamasha la Watoto wenye mahitaji maalum kwa Mwaka huu Wilhelmina Joseph amesema kufanyika kwa matamasha hayo kutasaidia kuondoa changamoto ya dhana potofu kwenye jamii kuhusu watoto wnye mahitaji maalum.
Mwalimu Emanuel Ibrahim kutoka Shule ya Jeshi la Uokovu ameipongeza Makumbusho ya Taifa kwa kuwakumbuka watu wenye mahitaji maalum huku Mwanafunzi Theresia Fredrick akisema tamasha hilo limewasaidia kuwaondolea upweke waliokuwa nao.
Tamasha hilo limekwenda sambamba na Kauli mbiu inasemayo haki sawa kwa wote hivyo wazazi na walezi wametakiwa kuepukana na imani potofu ya kuwaficha ndani watoto wenye mahitaji maalum