Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Juni 23, 2022 anafanya ziara ya siku moja katika mkoa wa Arusha na Tanga ambapo atashuhudia zoezi la awamu ya Pili ya wananchi takribani 117 kutoka kaya 27 wanaohama kwa hiari yao wenyewe kutoka katika eneo la hifadhi ya Ngorongoro kuelekea kijiji cha Msomera, Handeni
Mheshimiwa Majaliwa pia atakagua Makazi na miundombinu ya huduma kwa wananchi katika kijiji cha Msomera, Handeni mkoani Tanga
Pia Mheshimiwa Majaliwa atakagua alama zilizowekwa kubainisha eneo la hifadhi ya pori tengefu la Loliondo la Kilometa za mraba 1500.
Mheshimiwa Majaliwa amewapongeza wakazi hao kwa maamuzi yao ya kuhamia Katika kijiji cha Msomera ambapo amewahakikishia kwamba Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Samia. Suluhu Hassan ipo pamoja nao