Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akikabidhi Scanner kwa ajili ya kurahisisha zoezi la kubadilisha kumbukumbu za ardhi kutoka analogia kwenda digitali kwa Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Tabora Jabir Singano (wa pili kushoto) wakati wa ziara ya siku moja mkoani Tabora Juni 22, 2022. Wa pili kulia ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ardhi Tabora
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiangalia moja ya Scanner alizokabidhi kwa ajili ya kurahisisha kazi ya kubadilisha kumbukumbu za ardhi kutoka analogia kwenda digitali wakati wa ziara ya siku moja mkoani Tabora Juni 22, 2022.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akikagua zoezi la kubadilisha kumbukumbu za ardhi kutoka analogia kwenda digitali linalofanyika katika chuo cha ardhi Tabora wakati wa ziara ya siku moja mkoani humo Juni 22, 2022.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na wataalamu wanaofanya kazi ya kubadilisha kumbukumbu za ardhi kutoka analogia kwenda digitali katika Chuo cha Ardhi Tabora wakati wa ziara ya siku moja mkoani humo Juni 22, 2022.
Sehemu ya wataalamu wanaofanya kazi ya kubadilisha kumbukumbu za ardhi kutoka analogia kwenda digitali katika Chuo cha Ardhi Tabora wakimsikiliza Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (hayupo pichani) wakati wa ziara ya siku moja mkoani humo Juni 22, 2022.
Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Amos Zephania akizungumza wakati wa makabidhiano ya Scanner 50 kwa ajili ya kusaidia zoezi la kubadilisha kumbukumbu za ardhi kutoka analogia kwenda digitali katika chuo cha Ardhi Tabora Juni 22, 2022.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na wataalamu wanaofanya kazi ya kubadilisha kumbukumbu za ardhi kutoka analogia kwenda digitali katika Chuo cha Ardhi Tabora wakati wa ziara ya siku moja mkoani humo Juni 22, 2022. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)
………………………………
Munir Shemweta, WANMM Tabora
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amekabidhi Scanner 50 zenye thamani ya shilingi milioni 880 kwa kwa ajili ya kurahisisha zoezi la kubadilisha kumbukumbu za ardhi kutoka analogia kwenda digitali.
Dkt Mabula amekabidhi sehemu ya scanner hizo Juni 22, 2022 kwa Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Tabora Jabir Singano kwa niaba ya mikoa mingine wakati akiwa katika ziara yake ya siku moja katika mkoa wa Tabora.
Scanner zilizokabidhiwa zitasambazwa kwenye mikoa ya Mwanza scanner 9, Kagera 5, Tabora 6, Songwe 7, Dodoma 9, Shinyanga 7 na Mbeya 7 ambazo zote zinapelekwa kusaidia zoezi zima linaloendelea kwenye mikoa hiyo.
Akizungumza wakati wa kukabdhi vifaa hivyo, Dkt Mabula alisema kuwa, uamuzi wa wizara yake kutoa vifaa hivyo ni kutaka kuharakisha zoezi zima la kubadilisha kumbukumbu za ardhi kutoka analogia kwenda digitali.
‘’Tunatarajia sasa ninyi mliokabidhiwa jukumu hili la kubadilisha kumbukumbu kwa niaba ya wengine wote nchi nzima mtaendelea kuifanya kazi hii kwa weledi na kuongeza kasi ili tumalize na kuondokana na masuala ya mavumbi ya kwenye ‘mafile’ na tucheze na mfumo’’ alisema Dkt Mabula.
Kwa mujibu wa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, kwa wizara zoezi hilo lina maana zaidi kwenye mifumo kwa kuwa na uhalisia wa kutambua kumbukumbu ya mtu, kutokuwa na umilikishaji mara mbili, uchakataji nyaraka sambamba na kusaidia ramani kusomana.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Amos Zephania alieleza kuwa, yapo majadala ya muda mrefu wakati ulimwengu umebadilika na kwa kuliona hilo Wizara ya Ardhi imeona umuhimu wa kubadilisha kumbukumbu zake kutoka analogia kwenda digitali ili kwenda na wakati.
‘’Majalada mengine ni ya miaka 30 iliyopita lakini bado yanaisha, ulimwengu umebadilika na tumebaki kama tupo kanre ya 19 au 20, wizara imeona umuhimu wa kufanya zoezi la kubadilisha ramani hizi za upimaji, michoro ya mipango miji pamoja na nyaraka nyingine za umiliki kutoka nalogia kwenda digitali ili kwenda na wakati’’ alisema Zephania.
Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Tabora Jabir Singano alisema vifaa vilivyokabidhiwa vitarahisisha utendaji kazi na kuelezea utaratibu uliokuwa ukitumika kwenye ofisi yake kuwa ililazimu wataalamu wengine kufanya kazi had usiku.
‘’Tuliamua kuweka shift kwa sababu kuwaweka wataalamu wote asubuhi wakati vifaa vichache wengine wanakuwa hawana cha kufanya lakini baada ya kupata vifaa sasa watafanya kazi wakati mmoja’’ alisema Jabir Singano.
Ili kuongeza ufanisi katika utoaji huduma kwa kutumia mifumo ya TEHAMA wizara ya Ardhi imeendelea kuchambua, kufanya nakishi ya michoro (scanning) na kuhifadhi ramani na kumbukumbu za ardhi katika ofisi za Ardhi za mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini kwa awamu.
Hadi kufikia Mei 15, 2022 ubadilishaji wa michoro ya mipangomiji 5,649 yenye viwanja 1,758,424 na ramani za upimaji 31,500 zenye viwanja 598,000 katika halmashauri 38 umefanyika kutoka analogia kwenda digitali. Aidha utambuzi wa vipande vya ardhi 52,648 katika halamashauri za jiji la Dodoma na Manispaa ya Tabora , Shinyanga na Ilemela umekamilika.