Na Janeth Raphael – Dodoma
CHAMA cha Waajiri Tanzania kimetakiwa kutii sheria bila shuruti kwenye masuala ya Haki za wafanyakazi nchini, ikiwemo kuwasilisha michango ya mifuko ya jamii ya wafanyakazi wao kwa wakati.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Ajira,Vijana na wenye Ulemavu Prof.Joyce Ndalichako katika mkutano Mkuu wa 63 wa Mwaka wa Chama cha Waajiri Tanzania na Kongamano la waajiri (ATE)Jijini Dodoma ambapo amesema kuwa wizara yake haitosita kuchukua hatua kali kwa waajiri wasio tenda haki kwa wafanyakazi wao.
Aidha,prof Ndalichako amewataka waajiri nchini kulipa kwa hiyari wastaafu pensheni zao kabla orodha ya wadaiwa hao haijafika kwenye ofisi yake.
Hata hivyo Prof.Ndalichako amehitimisha kwa kuleta neema kwa Waajiri wa Sekta Binafsi huku akisema kuwa wapo katika hatua za mwisho za Mazungumzo na Sekta Binafsi kwa ajili ya kupandisha mishahara ya kima cha Chini kwa wafanyakazi wa Sekta Binafsi nchini.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa ATE Bi.suzanne Ndomba Doran ameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia suluhu hassan kwa kufanya mabadiliko mbalimbali katika sheria zinazogusa waajiri na kuongeza muda wa vibali vya kazi kutoka miaka Mitano mpaka miaka 8 kwa wale walioajiriwa pamoja na kuanzisha mfumo wa Kielektroniki wa kuomba vibali.
“Wote tunafahamu kuwa serikali ilitoa kima cha chini cha mshahara kwa sekta ya umma na mchakato wa kima cha chini cha mshahara kwa sekta binafsi unaendelea” alisema Bi.suzanne ndomba
Bi.suzanne ndomba ametoa wito kwa waajiri kutumia mkutano huo kutoa mapendekezo na Maoni juu ya yale yaliyopendekezwa na serikali kwa mwaka wa fedha ujao.
Dhima ya Mkutano Mkuu wa 63 wa Mwaka wa chama cha Waajiri Tanzania na kongamano la waajiri ni Kuboresha Sara za fedha na zakikodi ili kuongeza Tija na kuchochea Ukuaji wa Sekta za Kiuchumi.