Home Mchanganyiko WAWEZESHENI WASHAURI WA WANAFUNZI KUHUDHURIA MAFUNZO-PROF.KUSILUKA

WAWEZESHENI WASHAURI WA WANAFUNZI KUHUDHURIA MAFUNZO-PROF.KUSILUKA

0

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu    Mzumbe Prof. Lughano Kusiluka  akizungumza na washiriki wa wa mafunzo ya siku tatu ya Chama cha Washauri wa Wanafunzi Tanzania (TACOGA1984)  leo Juni 22,  2022, katika ukumbi wa mkutano wa  Taasisi  ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Jijini Arusha.

 

Mwenyekiti wa Chama cha Washauri wa Wanafunzi  Tanzania (TACOGA1984) Bi. Sophia Nchimbi akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya Chama cha Washauri wa Wanafunzi Tanzania (TACOGA1984)  leo Juni 22,  2022, katika ukumbi wa mkutano wa  Taasisi  ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Jijini Arusha.

Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango, Fedha na Utawala wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Dr. Shubi Kaijage akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya Chama cha Washauri wa Wanafunzi Tanzania (TACOGA1984)  leo Juni 22,  2022, katika ukumbi wa mkutano wa  Taasisi  hiyo Jijini Arusha.

Washiriki wa Mafunzo ya  Chama cha Washauri wa Wanafunzi  Tanzania (TACOGA1984) wakimsikiliza mgeni rasmi ambaye ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof.Lugano  Kusiluka (hayupo katika picha) wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya Chama hicho  leo Juni 22,  2022,  katika ukumbi wa mkutano wa  Taasisi  ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Jijini Arusha.

 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu  Mzumbe Prof. Lughano Kusiluka(katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na  Washauri wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu na Kati baada ya  kufungua  mafunzo ya siku tatu ya Chama cha Washauri wa Wanafunzi Tanzania (TACOGA1984)  leo Juni 22,  2022, katika ukumbi wa mkutano wa  Taasisi  ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Jijini Arusha.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu    Mzumbe Prof. Lughano Kusiluka (Katika Waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Serikali za Wanafunzi kutoka katika vyuo mbalimbali  baada ya  kufungua   mafunzo ya siku tatu ya Chama cha Washauri wa Wanafunzi Tanzania (TACOGA1984)  leo Juni 22,  2022, katika ukumbi wa mkutano wa  Taasisi  ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Jijini Arusha

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu    Mzumbe Prof. Lughano Kusiluka (Katikati Waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Chama cha Washauri wa Wanafunzi Tanzania(TACOGA 1984)  baada ya kufungua  mafunzo ya siku tatu ya Chama hicho   leo Juni 22,  2022, katika ukumbi wa mkutano wa  Taasisi  ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Jijini Arusha.

…………………………………..

Na Mwandishi Wetu.

Makamu Mkuu wa Chuo  Kikuu Mzumbe Prof. Lughano Kusiluka amezitaka Taasisi za Vyuo Vikuu na Vyuo vya Kati kuwawezesha Washauri wa Wanafunzi kuhudhuria mafunzo ya ushauri yanayoratibiwa na Chama cha Ushauri wa Wanafunzi Tanzania (TACOGA1984) ili kuwajengea uwezo katika utendaji wao.

Prof. Kusiluka  amesema hayo leo Juni 22, 2022, wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya Chama cha Washauri wa Wanafunzi Tanzania (TACOGA 1984) katika ukumbi wa mkutano wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Jijini Arusha.

“Mafunzo haya ni muhimu kwetu sote siyo tu kwa wanafunzi bali Jamii yetu yote, kupitia mafunzo haya  tunakuwa tumejenga Jamii bora kwa nchi yetu ” amesema Prof. Kusiluka

Aidha, ameongeza kuwa ni muhimu kwa washauri wa wanafunzi kuwa na mafunzo ya mara kwa mara ili waweze kutoa ushauri wenye kujenga na kuwapata wasomi bora wenye kutumikia taifa lao.

“wito wangu kwa wazazi tushirikiane kwa karibu na waalimu pamoja na washauri ili kuwalea wanafunzi katika mazingira mazuri yenye kuzingatia maadili mema” amesisitiza Prof. Kusiluka

Kwa upande wake Mwenyekiti wa TACOGA (1984) Bi. Sophia Nchimbi, ameeleza kuwa, lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo washauri wa wanafunzi waweze kufanya kazi zao kwa kufuata miongozo na kuwasaidia wanafunzi kuishi kwa kuzingatia maadili mema .

“Mada zitakazotolewa katika mafunzo haya ni 12 zikiwa na lengo la kuwajengea uwezo washauri wa wanafunzi katika masuala mbalilmabli ikiwemo  namna ya kuandika maombi ya   miradi, kuongea mbele ya hadhara na kuwashauri wanafunzi “ amesema Bi. Sophia Nchimbi

Naye mshiriki wa Mafunzo hayo ambaye ni Waziri Mkuu wa Serikali ya Wanafunzi kutoka Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni  Ndg. Ajubi Ally ameeleza kuwa, mafunzo hayo yatamsaidia katika kuwaongoza na kuwashauri wanafunzi wenzake namna ya kuishi kwa kuzingatia maadili na kuondokana na hofu pale wanapokutana na changamoto mbalimbali vyuoni.