Home Michezo TANZANIA NA QATAR KUSHIRIKIANA KATIKA MAANDALIZI YA MASHINDANO YA KOMBE LA DUNIA

TANZANIA NA QATAR KUSHIRIKIANA KATIKA MAANDALIZI YA MASHINDANO YA KOMBE LA DUNIA

0

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu (wa pili kushoto) akiongea na Balozi wa Qatar hapa nchini  Mh. Hussein Ahmad Al Homaid wa kwanza kulia) Juni 23, 2022 jijini Dar es Salaam kuhusu ushiriki wa Tanzania katika Mashindano ya Kombe la Dunia yanayosimamiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) ambayo yatafanyika nchini Qatar mwaka huu 2022.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu (kushoto) akiongea na Balozi wa Qatar hapa nchini  Mh. Hussein Ahmad Al Homaid  (kulia) Juni 23, 2022 jijini Dar es Salaam kuhusu ushiriki wa Tanzania katika Mashindano ya Kombe la Dunia yanayosimamiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) ambayo yatafanyika nchini Qatar mwaka huu 2022.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu (wa pili kushoto) akiwa katika kikao na Balozi wa Qatar hapa nchini   Mh. Hussein Ahmad Al Homaid(wa nne kulia) Juni 23, 2022 jijini Dar es Salaam kuhusu ushiriki wa Tanzania katika Mashindano ya Kombe la Dunia yanayosimamiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) ambayo yatafanyika nchini Qatar mwaka huu 2022.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Qatar hapa nchini  Mh. Hussein Ahmad Al Homaid  (kulia) Juni 23, 2022 jijini Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu (wa pili kushoto) akiwa katika kikao na Balozi wa Qatar hapa nchini  Mh. Hussein Ahmad Al Homaid (wa pili kulia) Juni 23, 2022 jijini Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu (kushoto) akiteta jambo na Balozi wa Qatar hapa nchini  Mh. Hussein Ahmad Al Homaid  (kulia) mara baada ya kikao chao Juni 23, 2022 jijini Dar es Salaam.

…………………………………………..

Na Eleuteri Mangi, WUSM-Dar es Salaam

Ujumbe wa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa ukiongozwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo Bw. Saidi Yakubu wamekutana na kufanya kikao pamoja na Balozi wa Qatar hapa nchini  Mh. Hussein Ahmad Al Homaid  kuhusu ushiriki wa Tanzania katika Mashindano ya Kombe la Dunia linalosimamiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA).

Viongozi hao wamefanya kikao cha pamoja Juni 23, 2022 katika Ofisi za Ubalozi wa Qatar hapa nchini Oyster Bay jijini Dar es Salaam kwa kuwa Mashindano ya Kombe la Dunia yatafanyika nchini Qatar mwaka huu 2022.

Katika mazungumzo yao viongozi hao wamekubaliana pande zote mbili kushirikiana katika maeneo mbalimbali ikiwemo kutumia wataalamu wa Tanzania kushiriki maandalizi kabla, wakati na baada ya mashindano hayo ikiwa ni fursa adhimu kwa Tanzania kujifunza namna ya kuandaa mashindano ya kimataifa.

Naibu Katibu Mkuu Bw. Yakubu pia amewasilisha kwa Balozi huyo maombi ya vijana wa Tanzania kupata fursa ya ajira za muda wakati wa mashindano hayo yatakayofanyika nchini Qatar.

Aidha, katika mazungumzo yao Naibu Katibu Bw. Yakubu ametumia fursa hiyo kumkaribisha Balozi wa Qatar hapa nchini        Mh. Hussein Ahmad Al Homaid    kushiriki kilele cha maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani ambayo yanaadhimishwa kwa mara ya kwanza duniani baada ya kuidhinishwa na Mkutano Mkuu wa 41 wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Novemba 23, 2021 ulipitisha azimio namba 41C/61 la kutangaza tarehe 7 mwezi Julai kila mwaka kuwa Siku ya Kiswahili Duniani.

Katika maadhimisho hayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi ambapo siku hiyo itaadhimishwa kuudhihirishia ulimwengu kuwa asili ya lugha ya Kiswahili ni Tanzania.

Kwa upande wake Balozi.  Mh. Hussein Ahmad Al Homaid amesema amepokea maombi hayo na kuahidi kuyafanyia kazi kwa kuzingatia uhusiano na ushirikiano mzuri uliyopo baina ya nchi hizo mbili.