Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani wa Kibiashara (FCC) Bw. William Erio (kulia) akibadilishana nyaraka na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) Bw. Godfrey Nyaisa mara baada ya kusaini mkataba wa ushirikiano.
kurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani wa Kibiashara (FCC) Bw. William Erio na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) Bw. Godfrey Nyaisa wakisaini mikataba hiyo
kurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani wa Kibiashara (FCC) Bw. William Erio akizungumza na waandishi wa habari baada ya kusaini mikataba hiyo. kulia ni Sylivesta Mpanduji Mkurugenzi Mkuu wa SIDO.
Baadhi ya watendaji wa Brela na FCC wakiwa katika hafla hiyo.
Tume ya ushindani wa Kibiashara (FCC) imesaini Makubaliano ya ushirikiano na Taasisi ya wakala wa usajili wa leseni na Biasahra BRELA pamoja na Taasisi ya kuendeleaza viwanda vidogo SIDO yanayolenga kuongeza utekelezaji wa kisheria wa majukumu ya taasisi hizo .
Akizungumza mara baada ya kusaini makubaliano hayo Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani wa Kibiashara (FCC) Bw. William Erio amesema makubaliano hayo yanalenga kuimarisha ushirikiano na utendajikazi wa pamoja katika kutatua changamoto mbalimbali za wawekezaji.
“Ushirikiano wa taasisi hizi unalenga kuimarisha na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa shughuli zinazolenga kuharakisha na kurahisisha uwekezaji nchini,” Amesema Erio
Akifafanua zaidi Bw. Erio amesema pia kulikuwa na hoja ya Mkaguzi Mkuu wa serikali (CAG) ambaye aliielekeza FCC na kuitaka kukaa pamoja na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) ili kutekeleza sheria inavyotaka kwa wale wanaotaka kuunganisha makampuni yao au kuuziana hisa kwa lengo la kuunganisha makapuni yao.
“Hivyo tumefanya hivi kujibu hoja ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) lakini pia kuhakikisha tunakaa pamoja na kuchukua hatua na wenzetu wa Brela katika kushughulikia suala la makampuni kuungana au kuuziana hisa kwa maana ya kushirikiana ili sheria iweze kufuatwa,” Amesema Erio.
Kwa hiyo ili kuhakikisha utekelezaji wa sheria hii unakwenda vizuri tunahitaji ushirikiano na kupeana mbinu ikiwa ni pamoja na elimu juu ya namna ya kushughulikia changamoto hizo.
Ameongeza kuwa sasa taasisi hizo zitaendelea na kampeni ya kutoa elimu ya namna ya kuunganisha makampuni ili wawekezaji wawe na uelewa wa namna ya kuunganisha ili kutekeleza matakwa ya kisheria na kuepuka adhabu zinazoweza kuwapata endapo wataunganisha makampuni yao bili kufuata utaratibu.
Naye Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) Bw. Godfrey Nyaisa amesema Migogoro ya kusajili alama za biashara ni mingi sana na unaweza usijue kwa sababu labda uko nje, lakini sisi ambao tuko katika maofisi tumekumbana na changamoto nyingi sana za wafanyabiashara kugombania alama za biashara.
Kikubwa hapa kuhusu ushirikiano huu ni kwamba kama wadau tulioungana kama Brela na FCC ni kuhakikisha tunafanya kazi hii pamoja kubwa tunaloenda kulifanya ni kutoa elimu zaidi kwa walaji ili waweze kuelewa na kuepuka makosa yasiyokuwa ya lazima kwa sababu ya kutojua sheria na utaratibu tu.