……………………..
Serikali imeridhia maombi ya baadhi wananchi wanaohama kwa hiyari yao kutoka hifadhi ya Ngorongoro kwenda katika maeneo mengine tofauti na Kijiji cha Msomera wilayani Handeni mkoani Tanga.
Hatua hii ya Serikali inatoa fursa kwa wananchi hao waendelee kupisha shughuli za uhifadhi katika eneo la Ngorongoro ambalo ni muhimu kwenye urithi wa dunia pia inazingatia misingi ya sheria na haki za binadamu.
Hayo yamesema na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana wakati akizungumza kwa njia ya mtandao kwenye mkutano wa kujenga uelewa kuhusu zoezi la uwekaji wa alama za mipaka katika Pori Tengefu la Loliondo na zoezi la uhamaji wa hiyari la wakazi wa Ngorongoro
Waziri Balozi Dkt. Chana amesema ni ruhusa kwa wakazi hao kuchagua kwenda kuishi mahala wanapo ona panafaa kwa kufuata taratibu zilizopo bila kuvunja sheria za nchi.
” Serikali yetu sikivu chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan inaendelea kujali maslahi ya wananchi kwa kutoa uhuru kwa wananchi walioamua kuhamia maeneo mengine kwa hiyari yao “. Amesisitiza Balozi Dkt. Chana.