…………………….
Viongozi mbalimbali wa Wanawake ndani ya Chama cha Mapinduzi wametakiwa kuiga mfano wa Mbunge wa Viti Maalum Wanawake Mkoa Njombe Mhe Balozi Dkt Pindi Chana ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, kwa kuchangia maendeleo kwenye maeneo yao na Tanzania kwa ujumla.
Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndg Gaudensia Kabaka, Mkoani Njombe kwenye mkutano wa Wanachama wa UWT Mkoa wa Njombe na Mwenyekiti huyo.
Katika mkutano huo Mama Kabaka alipokea na kugawa Pikipiki tano zilizotolewa na Mhe Balozi Dkt Chana, ili zisaidie kuongeza ufanisi wa shughuli za Chama na jamii kwa ujumla.