Afisa Elimu Mwandamizi wa Makumbusho ya Taifa Anamery Bagenyi akiwa Katika Soko la Kimataifa la samaki feri akiwaeleza wadau wa utalii kuhusu dhamira ya kufanya Utalii wa ndani ya jiji
Wadau wa utalii walipotembelea Katika Eneo la Mnara wa Askari Posta.
Wadau wa utalii walipotembelea Jumba la Kihistoria la Old Boma ambalo linasadikiwa ndio lilikuwa Jengo la kwanza la Gorofa na Kubwa kuliko yote Dar es salaam.
Afisa elimu Msaidizi wa Makumbusho Danford Majogo akiwaeleza wadau wa utalii kuhusu historia ya Jengo la Old Boma.
Mhifadhi Mwandamizi wa Kijiji cha Makumbusho Mr Wilberd Lema akiwaeleza wadau hao wa utalii tamaduni mbalimbali ambazo zinapatikana katika kijiji hicho
Muongoza Utalii Katika Kijiji Cha Makumbusho Ezbony Kashaga akiwaeleza watalii baadhi ya viumbe hai vinavyopatikana katika msitu uliopo ndani ya Kijiji hicho.
Mhifadhi Msaidizi wa Mambo ya kale Kunduchi Magofu Charles Bwaiye akiwaonyesha wadau wa utalii Magofu au makaburi waliyozikwa Masultani na mashekh Katika karne ya 15.
Picha ya Pamoja ya wadau wa utalii wakiwemo wanafunzi wa vyuo vya UDSM,IFM na Maafisa wa Makumbusho
…………………….
NA MUSSA KHALID
Watanzania wametakiwa kujiwekea mazoea ya kufanya Utalii wa ndani mara kwa mara ili waweze kujifunza na kujionea vivutio na Malikale za Kihistoria zilizopo Nchini.
Hayo yamejiri Leo jijini Dar es salaam wakati wa ziara ya utalii wa jiji kwa wadau mbalimbali ikiwahusisha wanafunzi Kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es salaam UDSM na IFM walipotembelea maeneo ya kihistoria yaliyopo katika Jiji hilo ambayo imeratibiwa na Makumbusho ya Taifa.
Watalii hao wa ndani kwa kushirikiana na Maafisa Kutoka Makumbusho ya Taifa wametembelea eneo la Kihistoria la Askaris Monument,Eneo la Mnazi Mmoja,Jengo la Kihistoria la Old Boma,Mnara wa saa,Jengo lililokuwa Dar es salaam Club ambalo kwa sasa ni Mahakama ya Rufaa,Kanisa La St Joseph na Azania Front ambayo yalianza kujengwa kuanzia miaka 1860’s mpaka Kwenye Magofu ya Kunduchi.
Akizungumzia ziara hiyo Afisa Elimu Mwandamizi wa Makumbusho ya Taifa Anamery Bagenyi amesema ni vyema Jamii ikajikita katika kufanya Utalii wa ndani mara kwa mara kwani kufanya hivyo ni kuendana na adhma ya serikali ya kukuza na kuendelea Utalii.
Amesema wanaendelea kumuunga Mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluh Hassama kupitia Royal Tour ambayo aliizondua Nchini majuma kadhaa yaliyopita lengo likiwa kuchochea sekta ya Utalii.
“Sisi Makumbusho ya Taifa lengo letu ni kuhakikisha tunatoa elimu dhidi ya maeneo mbalimbali ya kihistoria na Malikale Ili watanzania waweze kufahamu historia ya nchi yao.
Aidha amewataka Wananchi wa Dar es salaam na maeneo mengine kuepukana na Dhana ya kuwa kufanya Utalii ni mpaka kwenda mbugani kuangalia wanyama bali katika Mkoa huo umeshehemu vituo vingi vya kihistoria yakiwemo majumba ya kale,minara na masoko ya kihistoria.
Kwa Upande wao baadhi ya watalii hao wameipongeza Makumbusho ya Taifa kwa kuandaa program hiyo ya kufanya Utalii wa jiji huku wakiiomba kuifanya kuwa zoezi la mara Kwa mara kwani inasaidia kuwakumbusha watanzania kuifahamu Nchi yao ilipotoka na inapoelekea.