Na Mwandishi Wetu, Iringa
Wahariri wa Radio Jamii hapa nchini wameaswa kushiriki kikamilifu katika kuwaelimisha na kuwahamasiha wananchi ili waweze kushiriki Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Said Ameir leo Juni 16, 2022 wakati wa ufunguzi wa siku ya kwanza ya mafunzo kwa wahariri wa Redio Jamii yanayofanyika mjini Iringa kwa siku mbili.
” Baada ya mkutano na Wamiliki wa Vyombo vya Habari uliofanyika jijini Dar es Salaam, tumefanya mafunzo kwa Wahariri wa Mitandao ya Kijamii na sasa Wahariri wa Redio za Kijamii”, alisisitiza Bw. Ameir.
Akieleleza zaidi amesema kuwa mafunzo kwa makundi mbalimbali ya wadau ni sehemu ya utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Uelimishaji na Uhamasishaji.
Aidha, amesema kuwa wahariri hao wanalo jukumu kubwa katika kutoa elimu na kuhamasisha wananchi wote ili washiriki kikamilifu katika Sensa ya watu na Makazi Agosti 23, 2022.
Kwa upande wake mmoja wa watoa mada kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Hellen Hilary amesema Sensa ya Watu na Makazi itasaidia Serikali kupanga mipango ya Maendeleo kwa kuzingatia takwimu zitakazokusanywa.
Baadhi ya mada zitakazotolewa kwa Wahariri hao ili kuwajengea uwezo ni pamoja na; Sensa na Sheria ya Takwimu, Umuhimu wa Sensa ya Watu na Makazi na Maandalizi yake, Sensa na Mbinu za Uripoti kwenye Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 na Matumizi ya Mitandao ya Kijamii.
Sensa ya Watu na Makazi itafanyika Agosti 23, 2022 kote nchini ikilenga kusaidia kuongeza kasi ya maendeleo.
[6/16, 6:38 PM] Babu G.: NMB yakabidhi Vifaa vya Usafi – Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka ameagiza Jiji la Dodoma kuharakisha sheria ndogo ndogo za mazingira ili kuweka hali ya usafi katikati ya Jiji hilo.
Mtaka alitoa agizo hilo Kwa Naibu Meya wa Jiji la Dodoma, Emmanuel Chibago wakati wa kupokea vifaa vya kuhifadhia taka vilivyotolewa na benki ya NMB ili kusaidia utunzaji wa mazingira.
“Siku ile tulipata aibu kubwa, niliamua kuandika kwa mkono wangu kuomba vifaa hivi kwa benki ya NMB na leo wameleta,sasa naagiza vikabidhiwe kwa maandishi ili kila mmoja awe na wajibu wa kutunza na kuvifanyia kazi,” alisema Mtaka.
NMB wamekabidhi jumla ya mapipa 100 yenye thamani ya zaidi ya Sh20 milioni wakiahidi kuendeleza ushirikiano na mkoa ili kuweka mji katika hali ya usafi.
Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB, Juma Kimori alisema makabidhiano ya vifaa hivyo ni mipango ya benki hiyo katika kurudisha sehemu ya faida kwa wananchi baada ya kodi ambapo mwaka huu wametenga Sh.bilioni 2.9 ikiwa na ongezeko la 41% ukilinganisha na Sh.bilioni 2.05 za mwaka jana.
Kimori alisema walipokea ombi la vifaa vya kutunzia taka (dusty been) 350 kutoka kwa Mkuu wa Mkoa lakini kwa kuanza wametoa 100.
Awali Katibu Tawala wa mkoa Dkt Fatuma Mganga alisema baada ya makabidhiano hayo, sheria za usafi zitaanza kutekelezwa kwa mtu atakayetupa taka hovyo huku Dkt. Mganga akisema, awali ilikuwa ngumu kutekeleza sheria hiyo kwa sababu maeneo mengi hayakuwa na vifaa vya kuhifadhia taka hivyo kila mmoja alitupa kama anavyoona inafaa.