Mkuu wa Wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika ambayo yamefanyika katika viwanja vya Mwembeyanga wilaya humo.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Elihuruma Mabelya ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi ya mwanamke na mtoto akizungumza na wanahabari akiwaeleza umuhimu wa Siku ya Mtoto wa Afrika.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Tanzania Women Journalist Advocates For Children Right (TAWOJAC ) akizungumza na wanahabari katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika ambayo yamefanyika katika viwanja vya Mwembeyanga Wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam.Inspekta Blandina Ndunguru kutokea Dawati la Jinsia na watoto Changombe akizungumzia siku ya Mtoto wa Afrika
Baadhi ya wanafunzi na wadu mbalimbali ambao wamejitokeza kwenye sherehe hizo za maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika ambayo yamefanyika katika viwanja vya Mwembeyanga Wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam.
………………….
NA MUSSA KHALID
Jamii nchini imetakiwa kuwa na maadili ya kuimarisha ulinzi wa watoto kwa kutokomeza ukatili dhidi yao ili kuweza kutengeneza taifa bora la kesho.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika ambayo yamefanyika katika wilaya hiyo.
Mkuu wa Wilaya Jokate amesema kuwa ili kuhakikisha watoto wanapata ulinzi na haki zao serikali imefanya jitihada mbalimbali za kuunda mabaraza ya watoto kwenye mitaa na kata zao ili kutoa nafasi kwa watoto kujadili mambo yanayowahusu na changamoto zinazowakabili.
Aidha amewataka wazazi na walezi kuhakikisha wanaimarisha ulinzi kwa watoto pamoja na kuwapatia haki zao za msingi hatua itakayochangia malezi bora pamoja na kuimarisha makuzi ya akili .
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi ya mwanamke na mtoto ambaye ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Elihuruma Mabelya amesema umuhimu wa siku hiyo wanakwenda kuweka nguvu kuhakikisha haki za mtoto zinalindwa katika jamii mbalimbali.
Amesema katika kuhusiana na masuala ya ukatili wa watoto katika Halmashauri ya Temeke wamekuwa wakionyesha juhudi ya kuyatokomeza licha ya kutokea baadhi ya matukio lakini wameyadhibiti.
Naye Inspekta Blandina Ndunguru kutokea Dawati la Jinsia na watoto Changombe amesema ukatili wa watoto umekuwa ukijitokeza katika kutoka na jamii kutokuwa na elimu hivyo wamekuwa wakijitahidi kutoa elimu ili kupambana na ukatili huo.
Magreti Kyando ni Mwenyekiti wa Taasisi ya TAWOJAC amesema kwa mujibu wa takwimu ambazo zilitolewa zinaonyesha ukatili umekuwa ukiendelea huku baadhi ya wanafunzi wakiiomba serikali kuvidhibiti vitendo hivyo vya kikatili.