Kiongozi wa Timu ya Ukusanyaji wa Damu Wizara ya Afya Kanda ya Mashariki Peter Chami akizungumza na wanahabari katika zoezi la uchangiaji damu ambalo limefanyika katika Hotel ya Hyatt Regency Dar es salaam.
Kiongozi wa Timu ya Ukusanyaji wa Damu Wizara ya Afya Kanda ya Mashariki Peter Chami akimuandaa mchangiaji wa damu ambaye amejitokeza kuchangia damu.Meneja Masoko wa Hotel ya Hyatt Regency Dar es salaam Lilian Kisasa akizungumza na waandishi wa habari katika zoezi la uchangiaji damu ambalo limefanyika katika Hotel ya Hyatt Regency Dar es salaam.
Baadhi ya wachangiaji wa Damu ambao wamejitokeza katika zoezi la uchangiaji damu ambalo limefanyika katika Hotel ya Hyatt Regency Dar es salaam.(picha na Mussa Khalid)
…………………..
NA MUSSA KHALID
Imeleezwa kuwa kwa siku zinahitajika chupa 100 za Damu zitakazosaidia kuwaokoa watu wote wenye uhitaji wa damu katika maeneo mbalimbali nchini.
Akizungumza leo jijini Dar es salaam katika muendelezo wa zoezi cha uchagiaji wa damu Kiongozi wa Timu ya Ukusanyaji wa Damu Wizara ya Afya Kanda ya Mashariki Peter Chami amesema pia chupa moja ya Damu inauwezo wa kuwaokoa watoto watatu.
Chami amesema mahitaji ya Mpango wa Taifa wa Damu salama ni makubwa hivyo ni vyema wananchi wakaendelea kuhamasika kujitokeza kuchangia damu.
‘Mpango wa Taifa wa Damu salama tunajitahidi kukusanya damu na wengi wanajitokeza lakini bado mahitaji hayajajitosheleza hivyo wito wetu makampuni mbalimbali yaige mfano kwa mashirika mengine kama Kilimajaro hotel walipotuita sisi watu wa Mpango wa Taifa Damu salama kwa ajili ya kuchagisha damu zao’amesema Chami
Aidha Kiongozi huyo wa ukusanyaji wa Damu amesema kumekuwepo na changamoto kwa baadhi ya watu kutopenda kuchangia Damu wengi akiogopa sindano na wengine wakihofia majibu hali ambayo sio sahihi.
Amesema Mpango wa Taifa wa Damu salama lengo lao ni kuhakikisha wanandelea kutoa elimu kwa wananchi ili waweze kufahamu malengo na dhumuni hasa la uchangiaji wa damu kuwa ni kuwasaidia watanzania wenye uhitaji hasa waliopo katika hospitali mbalimbali nchini.
Kwa upande wake Meneja Masoko wa Hotel ya Hyatt Regency Dar es salaam Lilian Kisasa akizungumza wakati wakichagia damu amesema huo umekuwa ni muendeleo wa kuwa kuisaidia jamii kuanzia kipindi cha mwezi wan ne.
Amesema lengo lao ni kuhimiza watu kwa ajili ya utoaji wa damu salama ili wafahamu kuwa kufanya hivyo ni kuisaidia jamii ya kitanzania.
Nao baadhi ya wachangiaji wa Damu salama ambao ni wafanyakazi wa hoteli hiyo akiwemo Rukia Simba na Denis Sovokwetukia wamesema kilichowafanya waweze kutoa damu ni ili kuwasaidia na kuokoa maisha ya wananchi.
Hata hivyo watanzania wametakiwa kuendelea kujitokeza kwa wingi kuchangia damu yote yanajiri ikiwa ni kuelekea Maandimisho ya uchagiaji wa damu kwa mwaka huu ambayo yanakwenda sambamba na kauli mbiu isemayo ‘kuchagia damu ni kitendo cha mshikamano tuungane tuokoe maisha’.