Mkurugenzi wa kitengo cha dijitali na huduma za ziada Vodacom Tanzania PLC, Nguvu Kamando (katikati) akipokea tuzo ya Innovative Telco Company of the year 2021 toka kwa Afisa Uendeshaji wa Serengeti Bytes, Michael Mallya ambapo Vodacom walishinda tuzo hiyo kutokana na uwekezaji wake na uboreshaji wa mtandao na huduma bora kuzidi makampuni mengine ya mawasiliano kwenye tuzo za Tanzania Digital Awards zilizoandaliwa na Serengeti Bytes. Kulia ni Mkurugenzi wa huduma kwa wateja Vodacom Tanzania PLC, Harriet Lwakatare.
Mkurugenzi wa kitengo cha dijitali na huduma za ziada Vodacom Tanzania PLC, Nguvu Kamando (katikati) akinyanyua juu tuzo ya Innovative Telco Company of the year 2021 baada ya kuipokea kutoka kwa Afisa Uendeshaji wa Serengeti Bytes, Michael Mallya ambapo Vodacom walishinda tuzo hiyo kutokana na uwekezaji wake na uboreshaji wa mtandao na huduma bora kuzidi makampuni mengine ya mawasiliano kwenye tuzo za Tanzania Digital Awards zilizoandaliwa na Serengeti Bytes. Kulia anayepiga makofi ni Mkurugenzi wa huduma kwa wateja Vodacom Tanzania PLC, Harriet Lwakatare
Mkurugenzi wa huduma kwa wateja Vodacom Tanzania PLC, Harriet Lwakatare (katikati) akipokea tuzo ya Innovative Telco Company of the year 2021 kutoka kwa Afisa Uendeshaji wa Serengeti Bytes, Michael Mallya ambapo Vodacom walishinda tuzo hiyo kutokana na uwekezaji wake na uboreshaji wa mtandao na huduma bora kuzidi makampuni mengine ya mawasiliano kwenye tuzo za Tanzania Digital Awards zilizoandaliwa na Serengeti Bytes. Kushoto ni Mkurugenzi wa kitengo cha dijitali na huduma za ziada Vodacom Tanzania PLC, Nguvu Kamando
Mkurugenzi wa kitengo cha dijitali na huduma za ziada Vodacom Tanzania PLC, Nguvu Kamando na Mkurugenzi wa huduma kwa wateja Vodacom Tanzania PLC, Harriet Lwakatare wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa vodhashop makao makuu.
……………………………………….
KAMPUNI inayoongoza kwa huduma za teknolojia na mawasiliano nchini imetunukiwa tuzo nne na Kampuni ya Serengeti bytes kupitia programe ya Tanzania Digital Awards.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo June 7, 2022 Mkurugenzi wa Huduma kwa wateja, Harriet Lwakatare amesema kuwa Vodacomu Tanzania wamefurahia tuzo hizo na hiyo ndio inaonesha kazi kubwa unayofanywa na kampuni hiyo.
Amesema kuwa wametunukiwa tuzo nne (4) ambazo ni Tuzo ya Huduma bora kwa Mteja (best Customer care), ubunifu (Innovative telco of the Year), Mtoa huduma za Fedha kwa simu bora (Mobile Money, ‘M-Pesa’) pamoja na kampuni bora ya mawasiliano ya mwaka (Telco Company of the Year).
“Vodacom kama lengo letu lilivyo ni kutoa mawasiliano kwa wateja wetu wote tukitumia mbinu tofauti hasa ya kiteknolojia ya kisasa.” Amesema Harriet
Amesema kuwa tuzo walizotunukiwa leo zinoanesha kwamba wanafikisha bidhaa na huduma iliyobora kwa mteja kwa kutumia teknolojia ya kidigitali ambapo ulimwengu umegeukia kwa sasa na wateja wameweza kutuonesha kwamba wanastahili tuzo hizo.
Amesema tuzo hizo zimetolewa kwa kura za wananchi… Kwahiyo tunashukuru sana wananchi wote hasa hasa wateja wetu wa Vodacom kwa kuendelea kutuamini kwa huduma zote bora tunazozitoa.” Amesema Harriet