Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akihutubia wakazi wa shina namba 5 Nasa Ginnery, Kata ya Mwamanyili, Busega mkoani Simiyu.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akizungumza na Katibu wa NEC Siasa na Ushirikiano wa Kimataifa Kanali Ngemela Lubinga kwenye mkutano wa shina namba 5 Nasa Ginnery, Kata ya Mwamanyili, Busega mkoani Simiyu.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akimsikiliza Mwenyekiti wa shina namba 5 Ndugu Joseph Mabula Kasomi, Kata ya Mwamanyili, Busega mkoani Simiyu wakati akifungua mkutano huku akijadiliana jambo na Katibu wa NEC Siasa na Ushirikiano wa Kimataifa Kanali Ngemela Lubinga
Baadhi ya wakazi wa shina namba 5 Nasa Ginnery waliojitokeza kumsikiliza Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo ikiwa sehemu ya ziara ya kukagua uhai wa Chama pamoja na Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akimsalimia mmoja wa watoto waliofika na wazazi wao katika mkutano huo.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akiondoka kwenye mkutano mara baada ya kuzungumza na wanachama wa CCM shina namba 5 Nasa Ginnery, Kata ya Mwamanyili, Busega mkoani Simiyu.
……………………………………….
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo ameahidi kuwasiliana na Wizara ya Maliasili na Utalii ili kuona namna ambayo wizara hiyo inaweza kuchukua hatua za haraka kuwadhibiti Viboko hao ikiwemo kutoa kibali cha kuanza kuwavuna ili kupunguza idadi yao, kuepusha athari wanazozipata wananchi hatua ambayo amesema itasaidia kuondoa madhara kwa Wananchi.
Kufuatia uvamizi wa mara kwa mara wa Viboko hao kwenye makazi ya watu na kuhatarisha maisha ya Wananchi katika kata na Vijiji Vilivyopo Wilayani Busega mkoani Simiyu, Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ameahidi kulifikisha Suala hilo kwa Waziri wa Maliasili na Utalii ili atoe kibali cha kuanza kuvunwa kwa Viboko hao.
Chongolo amezungumza hayo Wilayani Busega ambapo yuko kwa ziara ya Ukaguzi ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2020-2025 ikiwa ni pamoja na Utekelezaji wa miradi ya Maendeleo.
Katibu Mkuu Chongolo amepokea taarifa ya Ripoti ya Uvamizi wa Viboko hao kutoka kwa Mbunge wa Busega Simon Songa pamoja na Diwani wa kata ya Mwananyile Timoth Mayala.
“Hatuwezi kuwa na viboko waliozaliana Sana, halafu ikawa ni mateso kwetu sisi, tunatamani viboko wawepo lakini wawe kwenye mazingira yanayoendana na sisi, wawe na uwezo wa kuishi na sisi na sio kutudhuru” amesisitiza Chongolo