Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akizungumza na wanachama wa CCM shina namba 3 Kijiji Cha Nyamikoma kata ya Kabita Busega mkoani Simiyu.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akizungumza na wanachama wa CCM shina namba 3 Kijiji Cha Nyamikoma kata ya Kabita Busega mkoani Simiyu kushoto ni Mwenyekiti wa Shina. Mamba 3 Nyamikoma Busumabu Mabula
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akikagua ujenzi wa kituo Cha Afya Cha Mkula wilayani Busega huku akipata maelezo kutoka Kwa Mganga mkuu wa wilaya ya hiyo Dk.Godfrey Mbagali. Wakati akiwa katika ziara yake wilayani Busega mkoani Simiyu.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akiendelea na ukaguzi wa kituo cha afya Mkula Busega.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akizungumza akimsikiliza Katibu wa NEC Siasa na Ushirikiao wa Kimataifa Kanali Ngemela Lubinga wakati alipokagua kituo Cha Mkula wilayani Busega mkoani Simiyu
Ukaguzi wa kituo hicho ukiendelea
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akipokelewa na Mwalimu Mkuu wa Sekondari ya Kabita Mwl. Michael Joseph Halali wakati aliowasili shuleni hapo kata ya Kabita Busega mkoani Simiyu kukagua madarasa yaliyojengwa Kwa fedhama UVIK0 19.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akiongozana na Mwalimu Mkuu wa Sekondari ya Kabita Mwl. Michael Joseph Halali wakati aliowasili shuleni hapo kata ya Kabita Busega mkoani Simiyu
Moja ya majengo ya madarasa ya UVIKO 19 yàliyojengwa Kwa fedha za UVIKO zililzotolêwa na serikai.
………………………………..
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) komredi Daniel Chongolo amekemea tabia ya baadhi ya watendaji wa serikali kuwapangia watumishi wapya vituo vya kazi kwa upendeleo.
Chongolo ameyasema hayo leo Juni 3, 2022 baada ya kupokea taarifa ya upungufu wa watumishi wa afya na Elimu katika baadhi ya vituo vya afya na Shule wilayani Busega.
“Tuache kupeleka watumishi wapya kwenye vituo vya kazi kwa upendeleo, kila mtu anawajibu wa kufanya kazi popote na wananchi kila mahala wanahitaji kuhudumiwa, acheni urasimu wapelekeni watumishi wapya kwenye vituo vya kazi vyenye uhitaji acheni kuwarundika Sehemu moja” amesisitiza Chongolo.
Chongolo yupo Wilayani Busega mkoani Simiyu katika muendelezo wa ziara yake inayolenga kukagua Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo kupitia Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020/2025.