Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Daniel Chongolo akiongozana na Mbunge wa Jimbo la Itilima mkoani Simiyu wakati akikagua mradi wa maji wa Nyamalapa akiwa kwenye ziara yake mkoani Simiyu Leo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Daniel Chongolo akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Ndugu David Kafulila wakati akifaanua jambo mara baada ya kukagua mradi wa maji wa Nyamalapa akiwa kwenye ziara yake mkoani Simiyu Leo. Kulia Hussein Yahya Meneja wa RUWASA wilaya ya Itilima.
Wananchi waliofika kwenye mradi huo wakimsimiliza Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo.
……………………………………..
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo amewataka wakala wa maji vijijini (RUWASA) wanapoendelea na shughuli ya kusambaza maji kwa kujenga matenki na kuchimba visima, wajenge matenki makubwa ambayo yatakuwa na uwezo pia wa kuhifadhi maji mengi kutoka ziwa Viktoria Ili kuiepusha serikali hasara nyingine ya ujenzi wa matenki kwani Mradi wa kusambaza maji ya ziwa Viktoria unaendelea na wilaya ya Itilima ipo katika mpango huo.
“Nitoe wito wangu kwa RUWASA, jengeni matenki ambayo yatakuwa na uwezo wa kubadilika baadaye tutakapokamisha mradi wa maji ya Ziwa Viktoria. Maji yatakuja mengi badala ya kutumia visima sasa tuunganishe matenki hayo na mfumo wa maji hayo kutoka ziwa Viktoria badala ya kuanza kujenga mapya.”
Sasa hivi ni lazima tujiandae kuwatayari kupokea maji yatakapofika kutoka ziwa viktoria, Sasa tunataka na Wana Itilima wapate maji kutoka Ziwa Viktoria,
“Hapa Itilima ni lazima maji ya Ziwa Vitktoria yafike, na Sio hapa tu yatafika Bariadi na Meatu, ambapo Maswa, Kishapu, Shinyanga mjini Kahama na maeneo mengine maji tayari yamefika, na hii ndio kazi ambayo anaifanya Mhe. Rais Samia kwa wananchi wote nchini”
Katibu Mkuu ametoa wito huo leo tarehe 2 Juni, 2022 akiwa katika Mkutano wa shina namba 7 kata ya Lagangabilili, baada ya kupata taarifa kutoka kwa Mkuu Wa Mkoa wa Simiyu David Kafulila kuwa Mkoa huo umepokea shilingi Bilioni 23 kwa ajili ya kujenga matenki ya maji na kuchimba visima.