Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Jenifa Omolo, hati maalumu kwa ajili ya kupanda na kutunza miti 2500 itakayopandwa katika mji wa Serikali Mtumba, baada ya kuzindua zoezi la upandaji miti katika Mji wa Serikali Mtumba (Magufuli City), jijini Dodoma.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, akipanda mti katika eneo la Mji wa Serikali Mtumba baada ya kuzindua zoezi la upandaji miti katika Mji wa Serikali Mtumba (Magufuli City), jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Jenifa Omolo, akipanda mti katika eneo la mji wa Serikali Mtumba, baada ya kuzinduliwa kwa zoezi la upandaji miti katika Mji wa Serikali Mtumba (Magufuli City), jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Jenifa Omolo, akimwagilia mti baada ya kuupanda, katika eneo la Mji wa Serikali Mtumba (Magufuli City), baada ya kuzinduliwa kwa zoezi la upandaji miti katika Mji huo, jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Jenifa Omolo, akizungumza baada ya zoezi la kupanda miti katika Mji wa Serikali Mtumba (Magufuli City), jijini Dodoma, ambapo alisema kuwa Wizara ya Fedha na Mipango itashiriki kikamilifu katika utunzaji wa miti 2,500 itakayo pandwa na kutunzwa na Wizara hiyo.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi.Mary Maganga, akifurahia jambo na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Jenifa Omolo, (kushoto) baada ya kuzinduliwa kwa zoezi la upandaji miti katika Mji wa Serikali Mtumba (Magufuli City), jijini Dodoma.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WFM, Dodoma)
……………….
Na. Peter Haule, WFM, Dodoma
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na MIpango, Bi. Jenifa Omolo ameahidi kuwa Wizara yake itapanda miti 2500 katika eneo la mji wa Serikali ulioko Mtumba ili kuhifadhi mazingira na kupendezesha mandhari ya mji huo.
Bi. Omolo ametoa ahadi hiyo baada ya kuongoza wafanyakazi wa Wizara hiyo kushiriki zoezi la upandaji miti lililozinduliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, katika Mji wa Serikali (Magufuli City) Jijini Dodoma.
Bi. Omolo alisema kuwa Mhe. Waziri Mkuu ameikabidhi Wizara yake hati maalumu kwa ajili ya kupanda na kutunza hiyo 2500 itakayopandwa katika eneo la Ofisi za Wizara kwenye mji huo wa Serikali.
“Kama Wizara tutajiunga na Wizara nyingine na nchi kwa ujumla kuhakikisha tunatunza miti na kupanda miti ya maua na ile itakayoainishwa na wataalam katika jengo jipya la Wizaraya Fedha na Mipango linalojengwa katika Mji huo wa Serikali”, alisema Bi. Omolo.