Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akimsikiliza Bi. Nice Munisi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Shinyanga DC wakati akitoa maelezo kuhusu Maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya wilaya hiyo mkoani Shinyanga.
Katibu Mkuu anatarajiwa kumaliza ziara ya mkoa Shinyanga leo tarehe 30 Mei, 2022 katika wilaya ya Kishapu ambapo atakagua na kuhimiza Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020 – 2025 pamoja uhai wa Chama.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akiongozana na Bi. Nice Munisi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Shinyanga DC wakati akikagua Maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya wilaya hiyo mkoani Shinyanga.
Moja ya majengo ya Hospitali hiyo ambayo tayari yamekamilika.
Baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wakimsimiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo wakati akiwahutubia mara baada ya kukagua hospitali hiyo.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akiwahutubia viongozi na wanachama wa CCM wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga DC.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akipokelewa na Wana CCM wa Old Shinyanga wakati alipowasili akitokea Wilayani Kahama.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mh.Patrobas Karambi akizungumza na wananchi wa Jimbo lake mara baada ya kumpokea Katibu Mkuu wa CCM ndugu Daniel Chongolo.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akiwasalimia wakazi wa kata ya Old Shinyanga waliojitokeza kumlaki
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akiwasalimia wakazi wa kata ya Old Shinyanga waliojitokeza kumlaki.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akipata maelezo kutoka Kwa Gaudioz Mwombeki Aifisa Mtendaji wa kata ya Lubaga wakati alipokagua ujenzi wa shule ya Sekondari ya Lubaga katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga DC mkoani Shinyanga.