Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo ameahidi kushinikiza upatikanaji wa fedha za dharura kugharamia ujenzi wa barabara ya Kolandoto mkoani Shinyanga hadi Meatu, Simiyu yenye urefu wa kilometa 53.
Chongolo ametoa ahadi hiyo alipofanya ziara katika Mkoa wa Shinyanga, baada ya Mbunge wa Jimbo la Kishapu, Boniface Ntondo kuomba barabara hiyo.
Kaimu Meneja wa TANROADS mkoani humo, Ferdnand Mdoe, amesema ukarabati wa barabara hiyo pekee huigharimu Serikali Sh.600 milioni kila mwaka na kwamba itakapotengenezwa gharama hizo zitaepukwa.