Mhe. Omar Ali Omar, Mbunge wa Wete, Pemba akizungumza na wanafunzi katika
Mhe. Agness Hokororo, Mbunge wa Viti Maalum, Mtwara.
Mhe. Noah Lembris, Mbunge jimbo la Arumeru Magharibi.
Meneja wa Sekta Isiyo Rasmi, Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bi. Rehema Chuma.
Afisa Mkuu Sekta Isiyo Rasmi, NSSF, Bi. Asha Sadick akitoa maelezo jinsi kujaza fomu ya kujiunga uanachama wa NSSF kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe
Mwanachuo akiweka dole gumba kukamilisha fomu aliyojaza ya kujiunga na NSSF.
Wanachuo wakifurahia burudani iliyokuwa ikitolewa na GNAKO.
Baadhi ya wanachuo wakijaza fomu za kujiunga na NSSF
Msanii wa Bongo Fleva, GNAKO akiburudisha na kutoa ushuhuda.
………………………………….
NA MWANDISHI WETU, MOROGORO
WANAFUNZI wa Chuo cha Mzumbe na Chuo cha Jordan Mkoani Morogoro wamehamasishwa kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba kwa kujiunga na Mfuko wa NSSF kupitia Mpango wa Taifa wa Sekta Isiyo Rasmi chini ya kampeni ya “Boom Vibes na NSSF” iliyotua mkoani Morogoro Mei 28, 2022.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na wanachuo hao, baadhi ya wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria ambao ni Mhe. Agness Hokororo, Mhe. Omar Ali Omar na Mhe. Noah Lembris ambapo kwa Ofisi ya Waziri Mkuu ikiwakilishwa na Frank Kilimba.
Wabunge hao walisema kuna faida kubwa sana ndani yake inapatikana kwa wanafunzi wa elimu ya juu kujiunga na kujiwekea akiba NSSF kwani itawasaidia katika kutafuta mitaji mbalimbali ya kibiashara.
Kwa upande wake, Meneja wa Sekta Isiyo Rasmi wa NSSF, Rehema Chuma aliwahakikishia kuwa hawatajutia uamuzi wa kujiunga na Mfuko huo kwani utawasaidia katika maisha yao ya sasa na baadaye.
“Ni muhimu wewe kama mwanachuo kuanza utamaduni wa kujiwekea akiba kupitia NSSF, ukianza kuweka akiba mapema itakuwezesha kuwa na akiba ya kutosha inayoweza kuwa mtaji wa biashara pindi utakapomaliza elimu yako.”
Alisema unapokuwa mwanachama wa NSSF unatakiwa kuhakikisha unachangia kiasi kisichopungua shilingi elfu ishirini (20,000/=) kila mwezi au zaidi na uwasilishaji michango ni rahisi kupitia mitandao ya simu na benki.
Rehema alisema Hifadhi ya Jamii ipo makhususi kwa ajili ya kuikinga jamii dhidi ya majanga mbalimbali hasa yale yanayosababisha upungufu wa kipato katika jamii zetu.”
“NSSF inatoa huduma za Hifadhi ya Jamii kwa makundi mawili ya wanachama, kundi la kwanza ni lile la wanachama walioajiriwa katika sekta binafsi ambao kwa mujibu wa sheria wanachangia asilimia 20% ikijumuisha makato ya asilimia 10% kutoka kwenye mshahara wa mfanyakazi na asilimia 10% kutoka kwa mwajiri,” alisema.
Aliongeza kuwa: “Kundi la pili ni la wanachama kutoka sekta isiyo rasmi yani mtu binafsi aliyejiajiri mwenyewe na anachangia NSSF kuanzia kima cha chini cha shilingi elfu 20,000/= kwa mwezi na ninyi wanafunzi mnaingia kwenye kundi hili.”
Kampeni hiyo ilipambwa na wasanii mbalimbali akiwemo msanii maarufu wa Bongo Fleva GNAKO ambaye aliwahi kuwa Mwnachama wa NSSF.
“Hata mimi nilikuwa mnufaika wa NSSF, kabla ya kuingia katika muziki nilikuwa nimeajiriwa Jijini Arusha, mwajiri wangu alikuwa ananikata sehemu ya mshahara wangu, kwa hakika nilikuwa sipendi kukatwa mshahara wangu lakini siku mkataba wangu wa kazi ulipomalizika niliamua kuendelea na harakati zangu za muziki ambapo nilichukua mafao yangu kutoka NSSF na yalinisaidia kulipia studio na hata video zangu za mwanzo,” alisema GNAKO.