Msemaji wa kampuni ya M-Bet Tanzania David Malley (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi Mshindi wa droo ya Perect 12 Baraka Lugwisha Shoki ambaye aliweza kubashiriki kwa usahihi matokeo ya mechi 12 za ligi mbalimbali duniani na kufanikiwa kushinda Sh168, 972,500.
Mshindi wa droo ya Perect 12 wa kampuni ya M-Bet Tanzania, Baraka Lugwisha Shoki katika pozi la furaha baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi yenye thamani ya Sh 168, 972,500. Shoki aliweza kubashiriki kwa usahihi matokeo ya mechi 12 za ligi mbalimbali duniani na kufanikiwa kushinda kiasi hicho cha fedha
……………………………………………………
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Mkazi wa mkoa wa Kagera, Baraka Lugwisha Shoki amejishindia kitita cha Sh 168,972, 500 baada ya kubashiri kiusahihi mechi 12 za mchezo wa Perfect 12 unaondeshwa na kampuni ya M-Bet Tanzania.
Shoki ambaye ni shabiki wa Simba, Geita Gold FC na Chelsea alisema kuwa haikuwa kazi rahisi kwa yeye kushinda kiasi kikubwa cha fedha hicho kutokana na ugumu wa kubashiri kwa baadhi ya timu zilizokuwa zinacheza.
Alisema kuwa mechi iliyompa wakati mgumu ni kati ya Dodoma Jiji FC na Namungo FC iliyochezwa uwanja wa Jamhuri, Dodoma na Dodoma Jiji FC kushinda.
Alifafanua kuwa kabla ya mechi hiyo, Namungo FC ilikuwa na matokeo mazuri na Dodoma Jiji FC ilikuwa na matokeo mabaya na ilifanya mabadiliko ya benchi lake la ufundi.
Alisema kuwa Namungo FC ilikuwa katika kiwango kizuri sana, lakini baada ya kuona Dodoma Jiji inacheza nyumbani, aliipa ushindi timu hiyo kwani isingekuwa rahisi kwao kuendelea kupoteza mechi hiyo.
“Baada ya Dodoma Jiji FC kuongoza, niliendelea kufanya maombi na nilitamani mwamuzi asiongeza muda kwani nilihofia Namungo FC wangesawazisha, hivyo nilichukia mwamuzi kuongeza dakika,”alisema Shoki.
“Sikuwa na wasiwasi mara baada ya kupigiwa simu na Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya M-Bet, Allen Mushi kuwa ni mshindi wa fedha hizo.
“Niliamini kuwa ni mshindi kwani mimi siyo mtu wa kwanza kushinda droo ya Perfect 12 ya M-Bet, nimewaona washindi wengi kupitia vyombo vya habari.
Shoki ambaye ni mwalimu wa hesabu katika shule ya Sekondari ya Kikukwe, Bukoba.
Alisema kuwa atazitumia fedha hizo kwa kuongeza mtaji katika biashara zake na nyingine kuzitumia katika kilimo na kusomesha ndugu zake.
Mkurugenzi wa Masoko wa M-Bet Tanzania, Allen Mushi alisema kuwa ataweza kubadili maisha yake kupitia mchezo wao wa Perfect 12.
Mushi alisema kuwa M-Bet itaendelea kuwa nyumba ya washindi kwa kuwazawadia mamilioni Watanzanja.
Mushi pia aliwaomba Watanzania wenye umri zaidi ya miaka 18 kuendelea kubashiri kwani Mei 31 watafikia kilele cha droo yao ya Zali la M-Bet ambapo watatoa washindi watatu, mshindi wa gari aina ya IST, pikipiki na sh milioni moja.
Alisema kuwa mpaka sasa wamewazawadia Watanzanja pikipiki 12 na washindi wengine 12 wamejishindia sh milioni Moja kila mmoja.