Home Mchanganyiko WAFANYABIASHARA WA MKAA PWANI WAASWA KUVUTA SUBIRA , WAENDELEE KULIPA TOZO KWA...

WAFANYABIASHARA WA MKAA PWANI WAASWA KUVUTA SUBIRA , WAENDELEE KULIPA TOZO KWA MUJIBU WA SHERIA- RC KUNENGE

0
Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
Mkuu wa mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge amewaasa wafanyabiashara na wabebaji wa mkaa wanaotumia bodaboda , wavute subira wakati wakiendelea kulipa tozo iliyopo kisheria ya sh.250 kwa kilo hadi hapo Waziri wa maliasili na utalii atakapofanya mabadiliko kulingana na mapendekezo yaliyotolewa.
Aidha ameeleza, viwango hivyo vya tozo vinatozwa kwa mujibu wa GN namba 59 ya January 28 mwaka 2020.
Akitolea ufafanuzi wa malalamiko ya baadhi ya wafanyabiashara hao , kuhusiana na madai ya tozo kubwa wanayolipa kwasasa kutoka 25,000 kwa gunia lenye kilo 100 na kulipia kwa sh.37,500, Kunenge alisema mkoa umeshapokea mapendekezo yote na watayafikisha kwa Waziri mwenye dhamana yafanyiwe kazi.
“Viwango hivi vya tozo vinatozwa kwa mujibu wa sheria ,Tunafahamu kumekuwepo mapendekezo hayo ,jinsi ya kukusanya tozo hizo , mapendekezo mbalimbali yametufikia na yapo ngazi ya mkoa Utaratibu unafanyika na yanashughulikiwa “
“Na sisi tukiwa watendaji wa Serikali tumefahamu Lazima tufuate taratibu ili tusiingie kwenye changamoto ya uvunjaji au ukiukwaji wa sheria”;alieleza Kunenge.
Alielezea ,anafahamu wananchi na wafanyabiashara Wana malalamiko Yao na Wajue Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ni sikivu itayafanyia kazi.
Kunenge alibainisha ,Lengo la Serikali Ni kuongeza mapato na kuwasihi wafanyabiashara hao wasikwepe ushuru kwani Ni chanzo Cha kushuka kwa mapato.
Vilevile mkuu huyo wa mkoa, alitoa Rai kwa wananchi kutumia Nishati mbadala na wasitegemee Sana matumizi ya mkaa kwasababu Kuna kiwango Cha miti ambacho hawawezi kuendelea kukata miti kwasababu ya athari ya tabia nchi.
Baadhi ya wafanyabiashara wa mkaa wanaofanya shughuli zao , Kibaha Vijijini akiwemo Hosea  Paulo  na Yasin Rajabu  ,wanaiomba Serikali mkoa na wizara husika kuangalia kwa uchungu tozo waliyopandishiwa kutoka ushuru wa 12,500 baadae TFS ikapandisha 25,000 na Sasa Bei ambayo inawaumiza kulingana na maisha Ni 37,500 .
Nae Yasini alibainisha kwamba ,licha ya hayo bei ya shamba nayo ni kubwa 90,000 wakati zamani walilipia 60,000 .
Kwa mujibu wa sheria ya misitu na.14 ya mwaka 2002 na kanuni zake mfanyabiashara wa mkaa anatakiwa kulipa sh.250 kwa kila kilo ya mkaa au 12,500 kwa gunia lenye kilo 50.