Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Ndg. Daniel Chongolo akipata maelezo kutoka Kwa Dr. Ernest Chacha Mganga Mkuu Halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga inayojengwa katika Kijiji Cha Ntobo A kata ya Ntobo ambapo serikali metoa jumla ya shilingi bilioni 1.74 kukamilisha ujenzi huo kama zinavyoonesha picha mbalimbali hapo chini.
Chongolo yuko katika ziara ya siku 9 akikagua uhai wa chama na miradi ya Maendeleo inayotekelezwa na serikali kupiitia ilani ya CCM ya mwaka 2020- 2025,
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Ndg. Daniel Chongolo akitoa maagizo kwa Dr. Ernest Chacha Mganga Mkuu Halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga baada ya kutembelea hospitali inayojengwa katika Kijiji Cha Ntobo A kata ya Ntobo ambapo serikali metoa jumla ya shilingi bilioni 1.74 kukamilisha ujenzi huo kama zinavyoonesha picha mbalimbali hapo chini.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Ndg. Daniel Chongolo akelekea kupanda gari mara baada ya kukagua majengo ya hospitali ya Halmashauri ya wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga inayojengwa katika Kijiji Cha Ntobo A kata ya Ntobo ambapo serikali metoa jumla ya shilingi bilioni 1.74 kukamilisha ujenzi huo
Baadhi ya Wana CCM wakiwa katika mkutano huo.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Ndg. Daniel Chongolo akipata maelezo kutoka Kwa Mganga Mfawidhi wa kituo Cha Afya Cha Isaka Kahama mkoani Shinyanga Dk. Samweli Mapula wakati alipokagua jlujenzi wa kituo hicho ambapo serikali imetoa jumla ya shilingi milioni akizungumza na wanachama wa CCM wa Kijiji Cha Ntobo A wakati alipozungumza nao alipomtembelea mjumbe wa shina.
………………………………..
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo amewaonya viongozi waliopewa dhamana na Chama, kuacha kueneza fitina na majungu dhidi ya wengine wakati wa uchaguzi wa ndani.
Ndg. Chongolo amesema hayo wakati akizungumza na Wana CCM katika shina namba 3 Kijiji Cha Ntobo A alipomtembelea mwenyekiti wa shina Hilo lililopo kata ya Ntobo.
Chongolo amesema CCM ina utaratibu, Katiba, Kanuni na miongozo iliyondaliwa vizuri, lakini amegusia kuwa “Tatizo lililopo ni baadhi ya wanaopewa dhamana kwenye maeneo kutokutenda haki. Marufuku kwa yeyote kueneza fitina, majungu, uongo na uzushi dhidi ya wengine wakati huu wa uchaguzi,” amesisitiza.
Katibu Mkuu ameongezaa kuwa, haiwezekani wakati wote tangu mwaka 2017 viongozi hao wamekuwa ndani ya CCM lakini hawakuwahi kuonywa wala kujadiliwa kwenye vikao vya maadili, iweje tuhuma hizo ziibuke sasa kipindi cha uchaguzi.
“Kwenye kikao cha maadili haitwi, kwenye kikao cha kuulizwa haitwi, kwenye kikao cha kuhojiwa haitwi, mmefika wakati wa uchaguzi vikao asubuhi mchana jioni. Ooh… huyu mbaya, huyu mlevi, huyu mrefu, huyu mfupi, huyu mnene, huyu mwembamba anakuhusu nini?” Katibu Mkuu amehoji.
Iwapo tuhuma hizo za kweli, amehoji kwanini hazikuibuliwa wakati mwingine na hatimaye waziibue kwenye uchaguzi.
Katibu Mkuu amesema huo ni ujanja ujanja wa kukata majina na kuzalisha viongozi wasio na sifa, ambapo amesisitikuwa jambo hilo halitavumiliwa ndani ya CCM.
Katika hatua nyingine, Kuhusu zao la Pamba, Katibu Mkuu amewaagiza wakulima kuhakikisha wanazalisha kwa ubora ili kutengeneza tija na kuwa na ushindani katika soko la kimataifa.
Amesema msimu wa zao hilo mwaka huu umeanza na bei ya Sh1,562 kwa kilo, ambayo ni zaidi ya ile ya mwaka jana, iliyokuwa Sh1,050.
Ili kuendelea kuwanufaisha wakulima wa zao hilo, amezitaka mamlaka husika kuhakikisha zinaendelea kusimamia bei ya zao hilo kwa maslahi ya wakulima nchini.
Katika ziara hiyo, pamoja na viongozi mbalimnali wa mkoa wa Shinyanga, Katibu Mkuu ameongozana na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndg. Ngemela Luhinga, ambapo ametembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya afya na barabara, pamoja na kushiriki mikutano ya Mashina.