…………..
NA MUSSA KHALID
Makumbusho ya Taifa kupitia Kituo chake cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni imeendelea kuunga mkono Juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuhamasisha utalii kwa kuanzisha onesho maalum la Sanaa Pamoja na Utalii Endelevu.
Imeelezwa kuwa onesho hilo ni sehemu ya program ya kila mwezi ya sanaa na wasanii (Museaum Art Explosion) kwa lengo la kutangaza utalii wa utamaduni na shughuli mbalimbali za sanaa ili kufungua fursa ajira.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga amesema Museaum Art Explosion inaendana na lengo la serikali la kuhamasisha utalii hasa katika kazi kubwa ya Royal Tour .
Dkt Lwoga amesema kwa kushirikiana na Nafasi Art Space wanaunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika kuutangaza na kufungua fursa mbalimbali za utalii wa Tanzania.
‘Tunaenda kufanya maboresho mbalimbali katika maonesho ya Kimakumbusho na vituo vya Malikale ili kuweza kuvutia watalii wengi zaidi’amesem Dkt Lwoga
Aidha Dkt Lwoga amesema mpango mkakati wa miaka mitano wa Taasisi hiyo 2021/22 -2022/26 wameainisha mipango mbalimbali ya kuongeza idadi ya watalii wa ndani na nje ya nchi na kuongeza mapato ya taasisi hiyo.
Awali akizungumza Mratibu wa sanaa za Jukwaani Kwame Mchauru amesema malengo yao ni kuburudisha na kuonyesha uwezo wa sanaa katika kuhamasisha na kuonyesha fursa za taaluma mbalimbali katika Nyanja ya ubunifu.
Kwa upande wao baadhi ya wasanii akiwemo Tadi Alawi na Liston Kimaro wamesema kuwa watahakikisha wanafanya onyesho lililobora hivyo wamewahamasisha wanachi kujitokeza kwa wiki.