Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani wa Kibiashara (FCC) Bw. William Erio akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuhitimisha kikao kati ya taasisi hiyo na Tume ya Ushindani Halali wa Biashara ya Zanzibar(ZFCC) kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani Halali wa Biashara Zanzibar (ZFCC) Mohammed Sija Mohammed.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani Halali wa Biashara Zanzibar (ZFCC) Mohammed Sija Mohammed akizungumza katika kikao hicho kushoto ni Ummy Muhamed Rajab Mkurugenzi Miungano ya Makampuni na Udhibiti wa Ushindani (ZFCC)
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani wa Kibiashara (FCC) Bw. William Erio akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuhitimisha kikao kati ya taasisi hiyo na Tume ya Ushindani Halali wa Biashara ya Zanzibar(ZFCC) katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani Halali wa Biashara Zanzibar (ZFCC) Mohammed Sija Mohammed na kushoto ni Ummy Muhamed Rajab Mkurugenzi Miungano ya Makampuni na Udhibiti wa Ushindani (ZFCC).
……………………………………….
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani wa Kibiashara (FCC) Bw. William Erio, amesema pamoja na suala la biashara kutokuwa la muungano, muingiliano wa kibiashara katika pande zote hizi mbili ni mkubwa na halina ubishi ,kwanza kwa wafanyabishara wenyewe lakini pia kuna wawekezaji waliowekeza katika pande zote mbili hivyo ili kutekeleza majukumu ya vikao katika kutekeleza majukumu yetu katika ushindani wa biashara na uzuiaji wa bidhaa bandia nchini.
Bw. William Erio ameyasema hayo leo wakati wa kuhitimisha kikao cha pamoja katika ya TUME ya Ushindani (FCC)na Tume ya Ushindani Halali wa Biashara ya Zanzibar(ZFCC) ambazo zimekutana katika kikao cha siku tatu Dar es Salaam kilichokuwa na lengo la kubadirishana uzoefu sambamba na kujengeana uwezo katika kukabiliana na suala la bidhaa bandia.
Pamoja na mambo mengine almesema kikao hicho pia kilikuwa na lengo la kuhakikisha masuala yote ya kibiashara katika pande zote mbili yanakwenda sawa na hivyo kusaidia ukuzaji uchumi kupitia sekta hiyo ya biashara licha ya kuwa suala hilo kutokuwa la kimuungano.
Amesema kupitia vikao hivyo wameweza kubadirishana uzoefu wa kutosha katika kuhakikisha malengo ya kuanzishwa kwa taasisi hizo zote mbili yaani FCC na ZFCC na matarajio ya viongozi waliowateua kwa lengo la kusimamia uchumi na biashara yanatimizwa hasa ikizingatiwa kuwa Serikali ya awamu ya sita imejikita kuhimarisha uwekezaji kama njia kuu kuongeza mitaji na kukuza uchumi kama ilivyo kwa Serikali ya awamu ya nane kule Zanzibar.
Amesema vikao hivyo vitakuwa endelevu, ili kujadiliana namna mbalimbali ambavyo watajipanga kuhakikisha Tanzania inanufahika na soko la Afrika Mashariki pamoja na ujio wa soko huru la Bara la Afrika kama Taifa moja wanaweza kujipanga ili kuliepusha kuwa soko la watu wengine badala ya kuwa mmoja wa wazalishaji.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani Halali wa Biashara Zanzibar (ZFCC) Mohammed Sija Mohammed amesema kipindi hiki ZFCC pia imeanza kufanya mapitio ya sheria zake kwa lengo la kuhakikisha Kasi ya udhibiti wa bidhaa bandia inaongezeka huku akishukuru ushirikiano uliopo baina ya FCC na ZFCC katika kukabiliana na bidhaa hizo.