Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro, leo akizungumza Jijini Dar es salaam kwenye hoteli ya Lamada wakati akifungua mkutano wa siku 3 wa masuala ya haki na usuluhishi wa migogoro ya kibiashara barani Afrika kwa njia mbadala.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Dk. Khatib Kazungu akizungumza Jijini Dar es salaam alipkuwa akimkaribisha Waziri Dk. Ndumbaro kwenye hoteli ya Lamada ili kuzungumza na kufungua mkutano wa siku 3 wa masuala ya haki na usuluhishi wa migogoro ya kibiashara barani Afrika kwa njia mbadala.
Dr. Mike Falke Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Ujerumani GIZ akizungumza katika mkutano huo.
Dr. Katrin Bornemann Mkuu wa Maendeleo na Ushirikiano Ubalozi wa Ujerumani akizungumza katika mkutano huo.
Picha mbalimbali zikionesha washiriki wa mkutano huo kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi
Picha ya pamoja.
……………………………………..
Uwepo wa Sheria mpya ya Usuluhishi wa migogoro kwa njia mbadala nje ya Mahakama ni hatua kubwa katika kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara nchini Tanzania.
Haya yamesemwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro, leo tarehe 24 Mei, 2022, Jijini Dar es salaam wakati akifungua mkutano wa siku 3 wa masuala ya haki na usuluhishi wa migogoro ya kibiashara barani Afrika kwa njia mbadala.
” Madhumuni makuu ya kupitishwa kwa Sheria ya Usuluhishi ni kuhimiza mbinu za utatuzi wa haraka wa migogoro bila kuingiliwa na mahakama” alisema Dkt. Ndumbaro
“Sheria ya usuluhishi tayari imepelekea kuanzishwa kwa Kituo cha Usuluhishi ( Arbitration Centre) ambacho tunalenga kiwe bora na chenye hadhi ya kuaminika kimataifa” Alisema Dkt. Ndumbaro
Aidha, Dkt. Ndumbaro amesema ni ukweli usiopingika kwamba kutokana na ongezeko la uwekezaji na biashara, idadi ya migogoro ya kibiashara ni lazima izuke. hivyo ni bora kutumia njia mbadadala kwa utatuzi wa haraka, wa gharama nafuu na wa haki kwa migogoro ya kibiashara, kila inapowezekana.
Usuluhishi mbadala wa migogoro duniani umekuwa chombo kikuu cha utatuzi wa majukumu ya kimkataba. Uzoefu wa kawaida ni kwamba michakato mbadala ya utatuzi wa mizozo huhifadhi na kuimarisha uhusiano wa kibinafsi na wa kibiashara.
Faida za msingi za mfumo wa Usuluhishi Mbadala ni wenye utaratibu; gharama ya chini na huondoa haraka migogoro. Kwa hivyo utaweza kusaidia kutatua migogoro mingi ya kibiashara ya ndani na kimataifa kwa manufaa ya pande zote kwa ubora, kuliko mchakato wa kawaida wa kisheria
Akizungumza kwa niaba ya Balozi wa Ujerumani, Dkt. Katrin Bornemann amesema Ujerumani kupitia Taasis yake ya GIZ itaendelea kushirikiana na Wizara ya Katiba na Sheria hususani eneo la kupata Haki kwa urahisi hasa wanawake na watoto.
Mwisho, Dkt. Ndumbaro amewashukuru GIZ kwa kutoa msaada wa kifedha na kiufundi katika mkutano huu.