Waziri Mku  Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipoweka jiwe la msingi la jengo la Ufundi Tower katika Chuo cha Ufundi Arusha, Mei 24, 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Saidi Issa ambaye ni Meneja wa Ktengo cha Uzalishaji, Chuo cha Ufundi Arusha kuhusu ujenzi wa Jengo la Ufundi  Tower wakati Waziri Mkuu alipoweka jiwe la msingi la jengo hilo jijini Arusha, Mei 24, 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la msingi la jengo la Ufundi Tower katika  Chuo cha Ufundi Arusha, Mei 24, 2022.  Wa tatu kushoto ni  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Innocent Bashungwa, wa tatu kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,  Profesa Carolyne  Nombo na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella. Kushoto ni Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo na wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Zelot Stephene. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea  zawadi ya picha yake iliyochorwa na Mwanachuo wa Chuo cha Ufundi Arusha, Michael  Felix  (kulia) wakati alipoweka jiwe la msing  la ujenzi wa jengo la Ufundi Tower katika Chuo cha Ufundi Arusha, Mei 24,2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Baadhi ya washiriki wa  hafla ya uwekaji wa  jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la Ufundi Tower katika Chuo cha Ufundi Arusha  wakipiga makaofi kumkaribisha  mgeni rasmi  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowasili  kwenye viwanja vya Chuo hicho jijini Arusha, Mei 24, 2022. (Picha na Ofisi ya Naziri Mkuu)

Baadhi ya washiriki wa  hafla ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la Ufundi Tower katika Chuo cha Ufundi Arusha  wakimsikiliza mgeni rasmi  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza kwenye viwanja vya Chuo hicho jijini Arusha, Mei 24, 2022. (Picha na Ofisi ya Naziri Mkuu)