Mariamu Samwel (38) Mkazi wa Ilalambuli,wilayani Magu, leo akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) mbuzi anaoufuga baada ya kuwezeshwa na TASAF kupitia mpango wa PSSN II.
Waandishi wa habari waliowatembelea wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya za Walengwa (PSSN II)wakifanya mahojiano na Mariam Samwel (38)
Mariam Samwel ambaye ni mlengwa wa mpango wa PSSN II akiwa amesimama upenuni mwa nyumba yake ya zamani.
Mnufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya za Walengwa (PSSN II) wilayani Magu,Mariam Samwel akiwa amesimm mbele ya nyumba yake aina ya sloap aliyoijengwa kwa fedha za TASAF.
Sunzu Peleka Makenye(75),mmoja wa walengwa katika Kitongoji cha Shinembo, wilayani Magu, akiwa mbele ya nyumba yake ya zamni
Sunzu Peleka Makenye akiwaonyeshA waandishi wa habari (hawapo pichani) mabaki ya nyumba aliyokuwa akiishi baada ya kuanguka mwak huu.
Mlengwa wa Mpango wa PSSN II, Sunzu Peleka Makenye akifungua mlango wa nyumba yake aliyoijengwa kutokana na uwezeshaji wa ruzuku ya TASAF.
Mlengwa huyo wa Mpango wa Kunusuru Kaya za Walengwa wa PSSN II,akiwa mbele ya nyumba aliyojengwa kwa kipato kilichotokn na mradi wa ufugaji wa ng’ombe na mbuzi kutokana na ruzuku ya TASAF.
…………………………………………………….
NA BALTAZAR MASHAKA,Magu
MFUKO wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Wilaya ya Magu,umetumia zaidi ya sh.milioni 700 kuwalipa watu zaidi ya 6,000 wa Mpango wa Kunusuru Kaya za Walengwa (PSSN II) ili kuzinusuru kaya hizo.
Mratibu wa TASAF wilayani humo Daniel Sanyenge amesema leo alipotebelewa na waandishi wa habari kuwa wanufaika wa mpango huo wa PSSN II katika vijiji 82 wilayani humo wengi wao wamenufaika kwa fedha hizo na kukuza uchumi wao na familia zao.
Amesema sh.milioni 750 zilipokelewa na kuwalipwa kwa walengwa 6,042 ili kuzinusuru kaya hizo katika vijiji 82 wilayani humo,baadhi yao wameboresha makazi yao kwa kujenga nyumba za bati,kufuga ng’ombe,mbuzi na kuku pamoja na kufanya miradi ya maendeleo.
Sanyenge amesema licha ya mafanikio baadhi ya walengwa wana changamoto ya matumizi ya fedha yasiyo sahihi,hivyo kupitia kamati za usimamizi wanapewa elimu watumie ruzuku hiyo kuongeza vipato vyao.
“Idadi kubwa ya walengwa wanaotumia ruzuku vizuri wanaendelea na wana hali nzuri kutokana na vipato vyao kuboreka,watoto wanapata huduma za afya na elimu pamoja na lishe bora,”amesema Mratibu huyo wa TASAF.
Kwa upande wake Sunzu Peleka Makenye (75), mkazi wa Kitongoji na Kijiji cha Shinembo,Kata ya Kahangara,amesema kupitia TASAF amepata sh. milioni 3.5 baada ya kuuza mifugo yake (ng’ombe watatu na mbuzi 10) na kujenga nyumba ya kuishi kwa matofali ya saruji na kuezeka kwa bati.
Amesema kabla ya kuingizwa kwenye mpango huu alikuwa akiishi kwenye nyumba ya nyasi,kipato cha sh.40,0000 alichopokea kutoka TASAF alitumia kiasi kuwekeza kwa kununua mbuzi kidogo kidogo na walipozaliana alikawabadilisha 10 kwa ng’ombe watatu.
“Nilikuwa nalala kwenye nyumba ya nyasi lakini TASAF imebadilisha maisha yangu sasa ni mazuri,nimejenga nyumba nzuri ya bati ya vyumba viwili na sebule,baada ya kuuza ng’ombe hao watatu kwa sh. milioni 2.1 na mbuzi 10 kwa sh. 600,000,” mama huyo kikongwe.
Naye Mariamu Samwel (38) Mkazi wa Kitongoji cha Ilalambuli,Kahangara,amesema maisha yalikuwa magumu,alilala njaa,hakuwa na godoro wala kitanda,aliishi na kulala chini kwenye nyumba ya nyasi,wakati wa mvua alinyeshewa kutokana na uchakavu wa paa la nyasi la nyumba yake, kabla ya kuingizwa kwenye mpango.
Amesema fedha za TASAF sh.38,000 fedha anazopokea amewekeza kwenye ufugaji wa kuku na mbuzi aliwaowanunua kwa sh.20,000 ,baada ya kuzaliana aliuza baadhi akanunua mabati akajenga nyumba.
Mariamu ameishukuru TASAF kuwa imemsaidia,amejenga nyumba na hali ni nafuu,anafuga kuku na mbuzi wapatao 14 wakiwemo kondoo, ametumia sh.55,000 kununua mtambo wa umeme jua (Solar) kwa matumizi ya mwanga nyumbani.
Mtendaji wa Kijiji cha Shinembo, Milembe Martin,amesema Sunzu ni miongoni mwa walengwa waliotumia ruzuku ya TASAF kwa weledi na kufanikiwa kujenga nyumba ya makazi kwa zaidi ya sh. milioni 3 hivyo kujikwamua kutoka kuishi maisha duni na umasikini.