Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Dkt. Mehmet Gulluoglu akikata utepe wakati alipozindua mashine ya kisasa ya Cone-beam Computerized Tomographic(CBCT) kwa ajili ya uchunguzi wa magonjwa ya kinywa na meno yenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni 200 iliyotolewa kwa Hospitali ya Muhimbili kama Msaada kutoka Serikali ya Uturuki wengine kulia ni Mkuu shule ya Kinywa na Meno MUHAS Dkt. Matilda Mtaya Mlangwa na Katikati ni Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo cha (MUHAS), Profesa Appolinary Kamuhabwa.
Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Dkt. Mehmet Gulluoglu akizungumza mara baada ya kukabidhi mashine hiyo.
Mkuu shule ya Kinywa na Meno MUHAS Dkt. Matilda Mtaya Mlangwa akitoa shukurani zake kwa Balozi wa Uturuki mara baada ya kupokea mashine hiyo.
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo cha (MUHAS), Profesa Appolinary Kamuhabwa akimshukuru Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Mh. Dkt. Mehmet Gulluoglu mara baada ya kupokea mashine hiyo.
Dkt. Mehmet Gulluoglu akijaribu moja ya kipimo cha kinywa mara baada ya kukabidhi mashine hiyo ya kisasa ya Cone-beam Computerized Tomographic(CBCT) kwa ajili ya uchunguzi wa magonjwa ya kinywa na meno.
Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Dkt. Mehmet Gulluoglu akikabidhi vyeti kwa wahitimu mbalimbali waliomaliza kozi ya matibabu ya kinywa kwa kutumia mashine hiyo kutoka kwa wataalam wa Uturuki.
Picha zikionesha baadhi ya washiriki wa tukio hilo wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa hafla ya makabidhiano.
Baadhi ya wataalam kutoka nchini Uturuki wakiwa katika hafla hiyo.
Picha za pamoja.
Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi, Muhimbili (MUHAS) kitengo cha Afya ya kinywa na Meno kimepokea msaada wa mashine ya kisasa ya Cone-beam Computerized Tomographic (CBCT) kwa ajili ya uchunguzi wa magonjwa ya kinywa na meno chenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni 200
Mashine iliyotolewa na serikali ya Uturuki, ni ya kwanza kupatikana katika hospitali za serikali hapa nchini na imeelezwa kuwa ni suluhisho kwa wagonjwa wanaosubiri muda mrefu kwa ajili ya uchunguzi wa kinywa na meno kwa kuongeza kasi ya kuwapima wagonjwa wengi zaidi na kuondoa msongamano wa kusubiri vipimo kwa muda mrefu.
Akizungumza mara baada ya kupokea mashine hiyo, leo Mei 20,2021 jijini Dar es Salaam, Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo cha (MUHAS), Profesa Appolinary Kamuhabwa amesema mashine hiyo ina uwezoo wa kupima na kutambua Kwa haraka magonjwa ya kinywa na meno
Profesa Kamuhabwa amesema uhusiano mzuri uliopo kati Tanzanaia na Uturuki ndio umewezesha kupatikana kwa mashine hiyo ya Kisasa ambayo inaenda kuwa msaada kubwa hospitalini hapo na kwa wanafunzi wa shule ya kinywa na meno.
Naye Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Dkt. Mehmet Gulluoglu ameahidi kuendeleza ushirikiano mwema katika kuimarisha sekta ya afya nchini huku mtaalamu wa magonjwa ya kinywa na meno wa hospitali hiyo Dkt.Karpal Sigh akiweka bayana ufanyaji kazi wa mashine hiyo.
Kwa upande wake, Mkuu shule hiyo nchini, Dkt. Matilda Mtaya amesema watu wengi wanasumbuliwa na matatizo ya fizi, meno kutoboka na harufu mbaya kinywani
Amesema, kupatikana kwa mashine hiyo kunaashiria mwanzo wa kiwango kingine cha uboreshaji wa mafunzo na umakini wa matibabu katika shule hiyo katika kujifunza na kufanya tafiti mbalimbali za magonjwa ya kinywa na meno.
Amesema, Chuo hicho tangu kuanzishwa kwake mwaka 1979 kimekuwa kikijitahidi kutoa huduma bora kwa wananchi wote na mafunzo ya kliniki kwa wanafunzi wa meno yanayopatikana
“Tangu kuanzishwa kwa Chuo hiki mwaka 1979, tumekuwa tukijitahidi sana kutoa huduma bora kwa watu wote.
Vile vile, tumekuwa tukijitahidi kutoa mafunzo bora zaidi ya kliniki kwa wanafunzi wa meno ndani ya njia zinazopatikana”
Amesema, mwaka 2014 chuo kilianzisha mfumo wao kidijitali wa taarifa za wagonjwa ambao ulijumuisha uwekaji wa mifumo ya picha yaani periapical x-rays and Orthopantomography (OPG) ambazo hata hivyo zilikuwa zikitoa picha za pande mbili tu ambazo hazitoshi kufanya uchunguzi sahihi na upangaji wa matibabu kwa ajili ya taratibu za kisasa za meno kama vile matibabu ya Endodontic, Implantology, na hata baadhi ya matukio ya kiwewe na matatizo ya viungo vya temporomandibular.
“Mashine hii inaifanya Shule yetu kuvuka hatua nyingine muhimu katika uwanja wa uchunguzi wa matibabu kwa Madaktari, Wagonjwa na wanafunzi wa kliniki ambao watafaidika sana kwa kutumia mashine hii.
Hii sio mara ya kwanza Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kunufaika na msaada wa vifaa tiba zinazotolewa na wahisani mbalimbali kuwezesha ikiwa ni sehemu ya kuunga juhudi za serikali kutoa huduma bora kwa Watanzania.