Benki ya NMB inaendelea kuupiga mwingi! Hivyo ndivyo unavyoweza kuelezea kutokana na hatua mbalimbali ambazo benki hiyo imeendelea kuchukua katika kusogeza huduma zake karibu na Watanzania.
Kwa kushirikiana na kampuni ya bima ya Britam, Benki ya NMB inatoa bima ya vyombo vya majini mahususi kwa ajili ya uvuvi (Mtumbwi/Jahazi) vinavyotumiwa na wavuvi wadogo wadogo, wa kati na wakubwa.
Bima hii ni kinga endapo chombo na vifaa vyake vitapata majanga kama moto, kuzama, kuvamiwa, kuibiwa, kugongwa au kugonga vyombo vingine.
Pia, kwa ajili ya mvuvi endapo atapata ajali akiwa kwenye shughuli za kivuvi ndani ya maji au kando kando ya mto, bwawa, ziwa au bahari.
Faida za ziada utakazopata katika bima hii ni;
• Kifo kitokanacho na ajali, bima italipa Tsh 2,000,000
• Ulemavu wa kudumu utokanao na ajali – Tsh 2,000,000
• Gharama za matibabu yatokanayo na ajali – Tsh 500,000
• Mkono wa pole kwa familia kama mteja atafariki na ajali- Tsh 200,000
Nani anaweza kukata bima hii?
– Wamiliki wa vyombo vya uvuvi
– Wavuvi walioajiriwa na mmiliki wa chombo
– Wavuvi wanaovua baharini, maziwa makubwa kwa madogo, mabwawa makubwa, mito mikubwa kama Pangani na mito mingine yenye samaki kama malagarasi, ruaha na kagera.
Unachohitaji ili kupata Bima hii;
✓ Nakala ya kitambulisho cha uraia au namba ya kitambulisho
✓ Barua ya utambulisho kutoka kikundi husika cha uvivu
✓ Nakala ya kibali cha uvivu kilichotolewa na idara ya uvivu ya wizara ya Mifugo na uvuvi
Kwa taarifa na maelekezo zaidi, tembelea tawi lolote la NMB au piga simu namaba 0800 002 002 BURE!
Umebima?- SiNgumuKiHivyo!