RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Viongozi wa Dini alipowasili katika viwanja vya Msikiti Mkuu wa Ijumaa Malindi Unguja Jijini Zanzibar kuhudhuria Hauli ya Alhabib Sheikh Ahmad bin Abubakar Bin Sumeyt,miaka 100 tangu kufariki kwake.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Maulamaa (Wanazuoni) katika hauli ya kumuombea Marehemu Alhabib Ahmad bin Abubakar bin Sumeyt kwa kutimiza miaka 100 tangu kufariki kwake hauli hiyo iliyofanyika katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa Malindi Unguja Jijini Zanzibar na kuhudhuriwa na Wanazuoni kutoka sehemu mbalimbali na Nje ya Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Maulamaa(Wanazuoni) katika eneo la kaburi la Marehemu Alhabib Ahmad bin Abubabar bin Sumeyt wakimuombea dua ikiwa ni hauli ya kutimiza miaka 100 tangu kufariki kwake,(kulia kwa Rais) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi,Alhabab Aliu Bin Mohammed Hapsi na Sayyid Ahmad Mwinyi Baba,