Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2022 Sahili Geraruma akishuhudia makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kheri James kwenda kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ludigija kwa ajili ya kukimbizwa katika wilaya hiyo.Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2022 Sahili Geraruma akijitambulisha kwa viongozi na watendaji wa IlalaViongozi na watendaji wa Ilala wakikabidhiwa Mwenge wa Uhuru kwa ajili ya kukimbizwa katika Wilaya hiyoMkuu wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ludigija akitolea maelezo ya miradi mbalimbali ya kimaendeleo ambayo Mwenge wa uhuru utapita katika wilaya hiyo.Moja ya Mradi wa Daraja la Ulongoni A ambalo limewekwa jiwe la msingi leo na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2022 Sahili Geraruma Vikundi vya Hamasa ambavyo vimeshiriki katika mbio za mwenge wa Uhuru Ilala.(picha na Mussa Khalid)
…………………..
NA MUSSA KHALID
Kiongozi wa Mbio za Mwenge mwaka 2022 Sahili Geraruma amewataka watendaji wa jiji la Dar es salaam na watumishi wa umma kufanya kazi kwa kuzingatia sheria na kanuni hususani katika utekelezaji wa miradi ya Maendeleo ili miradi hiyo iweze kukamilika kwa haraka na kuleta tija katika jiji hilo
Kiongozi huyo Mbio za Mwenge ametoa kauli hiyo Jijini Dar es salaam wakati Mwenge wa uhuru ulipokimbizwa Wilayani Ilala ukitokea katika Wilaya ya Ubungo na kuzindua pamoja na kuweka jiwe la Msingi kwenye miradi mbalimbali ambapo amesema miradi hiyo inatumia fedha nyingi za Serikali Kwa lengo la kuwanufaisha wananchi hivyo amesema ni muhimu kulawa na uwazi kwenye utekelezaji wake.
Aidha Geraruma licha ya kuwapongeza watendaji kwa kutekeleza miradi ya kimaendeleo pia amekemea kitendo cha baadhi ya watendaji katika halimashauri mbalimbali nchini kuficha nyaraka za miradi wakati wa kuikagua .
‘Mambo ambayo tumeshakataa ni suala la kuficha nyaraka za miradi na kila wakati tunaimba kuwa isifichwe na siyo vyema ikaacha hivyo unavyoacha wakati kiongozi anataka kukagua ni kupuuza maagizo ya viongozi’amesema Geraruma
Hata hivyo awali Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ludigija amesema katika Wilaya ya Ilala Mwenge wa Uhuru Kwa mwaka huu wa 2022 unatembelea miradi sita yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni sita.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Ukonga Jerry Slaa alipozungumzia mradi wa shule ya Bangulo amesema ni miongoni mwa miradi iliyokusudia kuwasogezea wanafunzi shule karibu na kuwapungiza adha ya kutembea umbali mrefu kufuata masomo.
Mwenge wa uhuru Kwa mwaka 2022 umebeba kaulimbiu isemayo “Sensa ni Msingi wa mipango ya Maendeleo, jiandae kihesabiwa tuyafikie Maendeleo” ambapo pia umebeba ujbe wa rushwa “Kuzuia rushwa ni jukumu letu sote.