………………………
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Kampuni ya FUJAN HEXINGWANG INDUSTRY ya nchini China iliyo wekeza hapa nchini kwa lengo la kujadili fursa za uwekezaji katika Sekta ya Utalii.
Akizungumza na wawekezaji hao Mhe. Chana amewaeleza kuwa Tanzania ina maeneo mengi ambayo yana fursa adhimu za uwekezaji hivyo milango ipo wazi kwa watu mbalimbali wa ndani na nje ya nchi kuchangamkia fursa zilizopo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Bw, Xu Xingda ameipongeza Serikali ya Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweka Mazingira rafiki ya uwekezaji na jitihada zilizo fanywa na Mhe Rais Samia za kutangaza Utalii kupitia Filamu Royal Tour, jambo lililo wahamasisha kuwa na nia ya kuwekeza katika Sekta hiyo.