Mkuu wa kitengo cha utetezi THRDC Wakili Leopold Mosha akieleza mafanikio ya mtandao huo katika miaka 10 iliyopita katika mkutano uliowakutanisha wadau wa haki za binadamu nchini wakifanya tathmini ya miaka kumi ya Mtandao huoMratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu kwa kanda ya Mashariki na Pwani na Mkurugenzi wa Shirika la C-SEMA Michael Marwa akizungumza wakati wa mkutano uliowakutanisha wadau wa haki za binadamu nchini wakifanya tathmini ya miaka kumi ya Mtandao huoMkurugenzi wa Taasisi ya Equality Growth (EFG) na Mjumbe wa THRDC Jane Magigita akieleza dhamira ya watetezi wakati wa mkutano uliowakutanisha wadau wa haki za binadamu nchini wakifanya tathmini ya miaka kumi ya Mtandao huo
Picha ya pamoja wadau wa haki za binadamu nchini
…………………………
NA MUSSA KHALID
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania-THRDC umesema utendelea kushirikiana na Serikali,katika kuhakikisha wanasaidia utetezi wa haki za binadamu kwa wananchi ili waweze kushiriki katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo.
Hayo yameelezwa leo jijini Dar es salaam na Wakili wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu –THRDC Nuru Maro wakati akizungumza katika mkutano uliokutanisha wadau wa haki za binadamu nchini wakifanya tathmini ya miaka kumi ya Mtandao wa Watetezi wa haki za binadamu nchini THRDC kujadili changamoto na mafanikio ya mtandao huo katika kuitumikia jamii.
Wakili Maro amesema katika miaka 10 ya THRDC wamefanikiwa kuongeza wanachama zaidi ya 200 nchi nzima lakini pia serikali imetambua mchango wa Watetezi katika upatikanaji wa huduma mbalimbali ikiwemo haki za binadamu.
Amesema malengo yao ni kuhakikisha wanafanya kazi kwa pamoja na wadau wote wa watetezi wa haki za binadamu,ikiwa ni pamoja na serikali,Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora ili kuweza kuwasaidia wananchi.
Aidha Wakili Maro amesema licha ya kuwa na mafanikio pia kumekuwepo na changamoto ikiwemo kutokuwa na mazingira salama ya utendaji wa kazi kwa sheria na sera zinazowaongoza,lakini pia kutokuwa na ushirikiano kwa viongozi wa mashirika wanaofanya kazi katika ngazi za chini hivyo ameiomba serikali kuboresha ushirikano kwa ajili ya manufaa ya nchi.
‘Sisi THRDC tumekuwa tukishirikiana na Mahakama zote Tanzania Bara na Zanzibar na hivi karibuni tunaingia makubalino na Mahakama ya Zanzibar baada ya kuona changamoto zinazokabili serikali ya Mapinduzi Zanzibar baada ya kuona changamoto ya masuala ya Kijinsia,haki za watoto kuvunjwa na baada ya kuona kazi kubwa inayofanywa na wanamtandao serikali ya mapinduzi ikakubalina na sisi tufanye kazi kwa pamoja’amesema Wakili Maro
Wakili Maro pia ameishauri Serikali kuridhia mkataba wa kimataifa wa watetezi wa haki za binadamu wa mwaka 1998 unaolenga kulinda usalama wa watetezi wa haki za binadamu nchini ili kuhakikisha wanafanya kazi katika mazingira salama ya kusaidia jamii.
Awali akizungumza Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu kwa kanda ya Mashariki na Pwani na Mkurugenzi wa Shirika la C-SEMA Michael Marwa amesema kwa tahmini waliofanya unaonyesha uhusiano unaendelea kuimarika baina ya Watetezi na Serikali tofauti na miaka ya nyuma.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Equality Growth (EFG) na Mjumbe wa THRDC Jane Magigita amesema watetezi wanasimama kwa ajili ya kuwatetea watu na nchini Tanzania kumekuwa na ufanisi mkubwa katika masuala ya utetezi wa kulinda haki za kibinadamu.
Hata hivyo imeelezwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluh Hassan ndiye anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 10 ya Mtandao wa Watetzi wa Haki za Binadamu Tanzania-THRDC
Mei 13 mwaka huu.