Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Nchini (TIRA) Dkt. Baghayo Saqware akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam akitoa taarifa kuhusu hatua zilizochukuliwa na mamlaka ya usimamzi wa bima kwa kampuni nne za bima nchini zilizokiuka mwenendo sahihi wa ulipaji madai na fidia kwa wateja.
Meneja wa Utekelezaji Sheria na Kushughulikia malalamiko Okoka Mgavilenzi akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam akitoa ufafanuzi kuhusu masuala ya Bima.
…………………..
NA MUSSA KHALID
Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Nchini (TIRA) imewataka watanzania kuendelea kutumia huduma za bima nchini na kutosita kupeleka Malalamiko yao kwa Kamishna wa Bima pindi wanapoona kampuni za bima haziwatendei haki.
Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es salaam na Kamishna wa Bima Dkt. Baghayo Saqware wakati akitoa taarifa kuhusu hatua zilizochukuliwa na mamlaka ya usimamzi wa bima kwa kampuni nne za bima nchini zilizokiuka mwenendo sahihi wa ulipaji madai na fidia kwa wateja.
Dkt Saqware amesema kampuni hizo ni pamoja na Kampuni ya Insurance Group of Tanzania (IGT), Kampuni ya Jubilee, Kampuni ya Bima ya Resolution na Kampuni ya Bima ya UAP ambapo zimekiuka kifungu 131(1)(2)(4) cha sheria ya Bima Na. 10 ya mwaka 2009 pamoja na marekebisho yake.
Amesema kwa nyakati tofauti kuanzia tarehe 01/10/2021 – 15/02/2022 Kamishna wa Bima amepokea malalamiko zaidi ya 48 dhidi ya kampuni ya Insurance Group of Tanzania (IGT) ambapo Lalamiko moja moja lilihusiana na kiwango kidogo cha fidia kilichotolewa kwa munufaika wa bima, Malalamiko nane ni kuhusu ucheleweshaji wa mchakato wa madai,na Malalamiko matatu yanahusisha kutakaa madai bila kuwa na msingi wa kuyakataa.
‘Pia, Mamlaka imebaini kuwa kampuni hii, imeanzisha upya uchunguzi wa baadhi ya malalamiko ambayo awali wayakubali na kutoa Hati ya Kukubali kulipa fidia, jambo ambalo linaleta dukuduku na wasiwasi wa mwenendo wa wataalam na nia ya utoaji haki kwa wateja’;amesema Dkt Saqware
Amesma Mamlaka inatoa faini ya kiasi cha Tsh 5,000,000.00 kwa Mwenyekiti wa Bodi ya IGT kwa kutoishauri na kutosimamia vyema Menejimenti ya kampuni hivyo kusababisha wateja na wananchi kukosa haki zao.
Aidha kuhusu Kampuni ya Jubilee Dkt Saqware amesema Kwa nyakati tofauti kuanzia tarehe 01/10/2021 – 06/05/2022 Ofisi ya Kamishna wa Bima imekuwa akipokea malalamiko zaidi ya 04 dhidi ya kampuni hii.
‘Kwa kuzingatia Sheria na taratibu za uendeshaji wa Biashara za Bima nchini, Mamlaka inachukua hatua nne ya kuiagiza Kampuni ya Jubilee kulipa kiasi chote cha 511,065.49 Euro kwa Wizara ya Maji kama ilivyoagizwa 9 katika kikao cha tarehe 18. Novemba 2022 ndani ya siku 14 kuanzia siku ya tangazo hili’ameendelea kusema Dkt Saqware
Vilevile kuhusu Kampuni ya Bima ya Resolution Dkt Saqware amesema katika nyakati tofauti imekuwa ikikagua na kushauri namna nzuri ya uendeshaji wa kampuni hii baada ya kuona uwezo wake wa kifedha unazorota kutokana na usimamizi mbovu, mienendo yasiyo ya kitaalamu na ukiukwaji mkubwa wa sheria na ufanyaji wa biashara ya bima ulifanywa na Wakurugenzi na Afisa Mkuu wa kampuni hii
Dkt Saqware TIRA Inatoa adhabu ya kiasi cha Tsh 5,000,000.00 kwa Wakurugenzi, Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hii kwa kila kosa la kutofuata taratibu za kibima hivyo kuchafua taswira ya soko la bima.
Hata hivyo kuhusu Kampuni ya Bima ya UAP Dkt Saqware anesena Kwa nyakati tofauti kuanzia tarehe 01/10/2021 – 06/05/2022 Kamishna wa Bima amekuwa akipokea malalamiko zaidi ya 04 dhidi ya kampuni hiyo hivyo ameiagiza kampuni hiyo kulipa fidia mara ndani ya siku 7 kuanzia tarehe ya taarifa.
Kwa upande wake Meneja wa Utekelezaji Sheria na Kushughulikia malalamiko Okoka Mgavilenzi amesema katika Biashara ya Bima Kampuni zinaongozwa na uaminifu kwa kuwa wanashughulikia vitu vinavyogusa maisha ya watu.
Imeelezwa kuwa TIRA Kutokana na jukumu la kulinda watumiaji wa bima yaani wananchi na kuendeleza soko, imetoa onyo kwa kampuni za bima nchini zitakazochelewesha ama kuchezea haki ya fidia ya mwananchi.