Naibu katibu mkuu wizara ya katiba na sheria Dkt. Khatibu Kazungu akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika kikao kilichokutanisha asasi za kiraia chenye lengo la kuhakiki na kutoa mapendekezo katika mpango kazi wa pili wa haki za binadamu.
Mratibu Taifa Mtandao Wa Watetezi Wa Haki Za Binadamu Nchini -THRDC Onesmo Ole Ngurumo akizungumza katika kikao hichokilichokutanisha asasi za kiraia.
Baadhi ya wanahabari ambao wameshiriki katika mkutano huo wakichukua matukio muhimu.
Picha ya pamoja
………………………….
NA MUSSA KHALID
Asasi za kiraia zinazoshiriki katika uhakiki wa mpango kazi wa pili wa kitaifa wa haki za binadamu zimetakiwa kuendelea kutoa ushirikiano kwa serikali na kufanya kazi kwa weledi ili kuhakikisha serikali inatimiza wajibu wake kukuza na kulinda haki za binadamu kwa wananchi wake.
Naibu katibu mkuu wizara ya katiba na sheria Dkt. Khatibu Kazungu ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza katika kikao kilichokutanisha asasi za kiraia chenye lengo la kuhakiki na kutoa mapendekezo katika mpango kazi wa pili wa haki za binadamu.
Dkt. Kazungu amezisihi asasi hizo kuendelea kutoa ushirikiano kwa serikali na kufanya kazi kwa weledi ili kuhakikisha serikali inatimiza wajibu wake kukuza na kulinda haki za binadamu kwa wananchi wake.
Amesema mpango kazi wa kwanza licha ya kuwa na mafanikio lakini pia ulikuwa na changamoto ikiwemo usimamizi na ufuatiliaji wa kina kwa kuwa kazi zote zilikuwa zinafanywa na chombo kimoja, hivyo kulemewa na shughuli nyingi hivyo Mpango Kazi wa Pili kumekuwa na mgawanyo wa majukumu.
‘Nawasihi muendelee kutoa ushirikiano, kufanya kazi kwa weledi kwa kujituma na kwa kutambua kwamba zoezi hili ni nyeti na ni la muhimu kwa kuwa ni mfumo muhimu katika kuhakikisha Serikali inaitimiza wajibu wake wa Kikatiba wa kukuza na kulinda haki za binadamu na haki za watu kwa wananchi wake’amesema Dkt. Kazungu
Kwa upande wake Mratibu Taifa Mtandao Wa Watetezi Wa Haki Za Binadamu Nchini THRDC Onesmo Ole Ngurumo amesema katika kuadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwa mtandao huo hivyo wamekuwa wenyeji wa kikao hicho ikiwa ni kuendelea na jukumu la uboreshaji wa hali ya haki za binadamu nchini.
Baadhi ya wadau wa asasi za kiraia walioshiriki katika kikao cha mpango kazi wa pili wa haki za binadamu akiwemo Evelyne Senge kutoka Save The Mother and Children Tanzania pamoja na Mwanachama wa THRDC Samwel Sokolo wamesema kuwa na mpango wa pamoja baina ya serikali na asasi za kiraia ni chachu katika kusukuma gurudumu la maendeleo ya kijamii, kisiasa na kiuchumi.
Mpango Kazi wa Kitaifa wa Haki za Binadamu ni mwitikio wa mapendekezo yaliyotolewa na Mkutano wa Dunia kuhusiana na Haki za Binadamu uliofanyika Vienna mwaka 1993 ambao uliazimia nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa ziwe na Mpango Kazi wa Haki za Binadamu ambapo Oktoba 2008 Tanzania ilianza mpango kazi wa kwanza.