Kaimu Mkurugenzi wa Chuo cha Furahika Education Tanzania Dkt. David Msuya akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu mafunzo kozi ya uuguzi ngazi ya cheti kupitia mradi wa Msaidie Mama Mjamzito.
……………….
Chuo Furahika Education Tanzania kilichopo Buguruni jijini Dar es Salaam kupitia mradi wa Msaidie Mama Mjamzito wamewataka watanzania kuchangamkia fursa ya kujiunga na mafunzo ya kozi Uuguzi (Nursing) ngazi ya cheti yanayotolewa bure bila gharama yoyote kwa wanafunzi watakaofanikiwa kujiunga na chuo hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi wa Chuo cha Furahika Education Dkt. David Msuya, amesema kozi hiyo ya uuguzi itatolewa kwa muda wa mwaka mmojo, huku robo tatu ya wahitimu watakwenda kufanya kazi katika mradi wa Msaidie Mama Mjamzito.
“Robo tatu ya wahitimu wa ngazi ya cheti watakwenda vijijini kufanya kazi katika mradi wa Msaidie Mama Mjazito kwa kufanya kazi mbalimbali kupitia taaluma yao kwa kuwasaidia wagonjwa ikiwemo kugawa dawa” amesema Dkt. Msuya.
Dkt. Msuya ameeleza kuwa sifa ya wanafunzi wanaoitajika kujiunga na mafunzo ya uuguzi ni vijana wa jinsia zote wenye umri kunzia miaka 16 hadi 25 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania.
“Sifa ya wanafunzi ili ajiunge na chuo lazima amemaliza kidato cha nne, na awe amepata Biology alama D, pia Physics au Chemistry awe amepata alama D, na mafunzo yanatarajia kuanzia mwezi huu tano mwaka 2022” amesema Dkt. Msuya.
Amefafanua kuwa wazazi wanatakiwa kuchangamkia fursa ya kuwapa elimu vijana wao kwani itawasaidia katika maisha yao na kupiga hatau katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo.
“Sisi tunatoa mafunzo bure bila kulipa ada, wanafunzi anachangia gharama ndogo za mtihani, lengo ni kuwasaidia wapate elimu, kuna watu wanatumia fedha nyingi kuwapa elimu watoto wao” amesema Dkt. Msuya.
Chuo cha Furahika Education kimesajili na VETA na wanatoa kozi mbalimbali bure bia kulipa Ada, hivyo wananfunzi wanachangia ada ya mitihani wanayofanya ili aweze kupata cheti.
Lengo la Chuo ni kuendeleza watoto wa kike na vijana kuwapa ujuzi mbalimbali kwaajili ya mafanikio yao na familia kwa ujumla.
Katika hatua nyengine amempongeza Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Samia suluhu Hassan kwa Filamu ya Royal Tour kwani amefanya jambo nzuri lenye faida kwa Taifa.
“Kupitia Royal Tour baada ya miaka 10 ijayo tutapiga hatua kubwa katika maendeloe sekta ya Utalii na kutengeneza historia kubwa” amesema Dkt. Msuya.