Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege Tanzania Jeremia Shila wakati akitoa taarifa ya kukamatwa kwa Raia mmoja wa China aliyekutwa na vidani na bangili vilivyotengenezwa kwa meno ya tembo vikiwa na tahamani ya Tembo mzima
………………….
Jeshi la polisi Viwanja vya Ndege Tanzania limesema litahakikisha linawatia nguvuni na kuwafikisha katika vyombo vya sheria wale wote wanaojihusisha na kusafirisha madawa ya kulenya na nyara za Serikali katika uwanja wa ndege wowote hapa nchini.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege Tanzania Jeremia Shila wakati akitoa taarifa ya kukamatwa kwa Raia mmoja wa China aliyekutwa na vidani na bangili vilivyotengenezwa kwa meno ya tembo vikiwa na tahamani ya Tembo mzima .
Kamanda Shila amesema mtuhumiwa huyo Raia wa China amefahamika kwa jina la Dong Weijuan (44) alikuwa akisafiri kwenda Bang kok Thailand ambapo alikamatwa katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julias Nyerere ( JNIA).
‘Raia huyo mwenye umri wa 44 aliyekuwa akisafiri kwa ndege ya Qatar mruko namba QR 1499 majira ya saa 10:00kwenda BANGKOK,THAILAND akiwa na vidani kumi na bangili moja vilivyotengenezwa kwa meno ya Tembo vyenye uzito wa gramu 110,pia alikutwa na bangili nyingine moja iliyotengenezwa na manyoya ya mkia wa Tembo (Singa) vyote vikiwa na thamani ya tembo mzima’amesema Kamanda Shila
Katika tukio lingine Kamanda Shila amesema jeshi la Polisi Viwanja vya ndege limefanikiwa kumkata Raia mmoja wa India aliyefahamika kwa jina Paokholen Lhungdim ( 23) akiwa na madawa ya kulevya aina ya HEROIN yenye uzito wa Kg 17 .40.
Sanjari na hayo Shila amesema katika msimu huu wa Sikukuu za Eid El Fitri jeshi hilo limejipanga vizuri katika kuimarisha ulinzi maeneo yote ya Viwanja vya ndege huku akiwaomba wananchi waishio karibu na Viwanja vya ndege kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi katika jukumu la ulinzi.