Na. AsilaTwaha, OR- TAMISEMI
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Prof. Riziki Shemdoe amewapongeza wanamichezo wa TAMISEMI Sports Club kwa kushika nafasi za juu katika michezo ya Mei Mosi na kuwaambia nafasi hizo zinadhirisha kuwa, ushiriki wao katika michezo ulikuwa ni wakujituma katika kuipambania TAMISEMI.
Prof. Shemdoe
amesema hayo leo wakati akipokea kombe la timu hiyo ambapo Timu ya Tamisemi Sports Club Riadha inaongoza kuwa washindi wa jumla wa michezo ya Mei Mosi kwa Mwaka 2022 na kupata kombe la ushindi na midali akiendelea kusema, hata mchezo wa football kushika nafasi ya pili inaonesha mapambano yalikuwa ni yenye kuonesha utafutaji wa kuwa mabingwa wa jumla wa mchezo huo.
“Nimefurahi sana TAMISEMI ni kubwa kwa kuonesha ushiriki wa kucheza mchezo wa riadha, kamba, football, kurusha tufe,baiskeli na kucheza karata inaonesha wazi kuwa ninyi niwapambanaji niendelee kuwaomba endeleeni kujituma na sisi viongozi wenu tutaendelea kuwaunga mkono kwa kuwa pamoja nanyi kwa kuhakikisha mnaendeleza michezo ikiwa ni pamoja na kuzingatia sheria, kanuni taratibu na nidhamu wakati wote wa michezo yenu” amesema Prof. Shemdoe
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Victor Kategere awali amesema, pamoja na changamoto za kimchezo amemueleza Prof. Shemdoe timu ya TAMISEMI inauwezo mkubwa na endapo itaendelea kusimamiwa itafika mbali amesema mapambano walionesha tangia mwanzo wa michezo inastahili kuendelea kusapotiwa kwani michezo ni moja ya kujenga mahusiano mazuri, ajira lakini pia hujenga afya.
Naye Katibu wa TAMISEMI Sports Club Alex Morice ameushukuru uongozi wa Ofisi ya Rais TAMISEMI kuendelea kuisimamia timu hiyo na kuhakikisha timu hiyo inafikia malengo yake pia ameomba uongozi huo uendelee kuisapoti kwani timu yao ya netiboli inategemea kwenda nchini Kampala mwezi Mei, 2022 kwa ajili ya mshindano Club Binjwa Afirka Mashiriki.
Timu ya Tamisemi Sports Club riadha inakuwa mshindi wa jumla kwa sikuku ya wafanyakazi Mei Mosi mwaka 2022 na kutegemewa kupatiwa kombe la ushindi na mgeni rasmi ambapo inatarajiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluh Hassan.